Loading...

WAZIRI JAFO: Wakuu wa Wilaya Simamieni kazi zinazofanywa na TARURA

Loading...
WAZIRI JAFO: Wakuu wa Wilaya Simamieni kazi zinazofanywa na TARURA - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa WAZIRI JAFO: Wakuu wa Wilaya Simamieni kazi zinazofanywa na TARURA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : WAZIRI JAFO: Wakuu wa Wilaya Simamieni kazi zinazofanywa na TARURA
link : WAZIRI JAFO: Wakuu wa Wilaya Simamieni kazi zinazofanywa na TARURA

soma pia


WAZIRI JAFO: Wakuu wa Wilaya Simamieni kazi zinazofanywa na TARURA

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mh. Selemani Jafo amewaagiza Wakuu wa Wilaya wote nchini kusimamia  kazi zinazofanywa na Wakala wa Barabara Vijijini na Mijini (TARURA)  ili kuleta matokeo tarajiwa  katika kukuza ustawi wa kiuchimi nchini.
Akifungua kikao cha Wakuu wa Wilaya nchini kote, Mhe. Jafo amewataka Wakuu wa Wilaya kwenda kusiamamia barabara hizo kwa ukaribu ili barabara zitakazo jengwa ziwe na ubora na zitakazo dumu kwa muda mrefu.
Mhe. Jafo amewaambia wakuu hao kuwa uanzishwaji wa Wakala utainua chachu ya uzalishaji wa mazao kutokana na usafiri wa uhakika, ambapo mkulima atakuwa na uhakika wakusafirisha mazao, lakini pia kupunguza gharama za usafiri lakini pia kuboresha hali za maisha za watanzania.
Amesema Serikali imekuwa na changamoto kubwa sana ambapo wakandarasi wanaopatiwa kazi za ujenzi wa barabara kutokuwa waaminifu na kujenga chini ya kiwango, rushwa , hivyo ni kazi ya Mkuu wa Wilaya kusimamia ili kubaini mapungufu hayo kwa haraka na kuokoa fedha za Serikali.
Amesema kuwa baada ya kuifahamu TARURA ni jukumu lao kuibua maovu kwa wafanyakazi wanaofanya maovu ili waweze kuchukuliwa hatua za kinidhamu kwa kufuata sheria na taratibu za utumishi wa umma.
Amesema kuwa Wakuu wa Wilaya ni wawakilishi wa serikali katika maeneo yao, hivyo wanawajibu wa kusimamia kwa ukaribu zaidi katika usimamizi wa mradi ya Ujenzi wa Barabara nchini kwa kuzingatia kuwa asilimia 43 za barabara zinasimamiwa na TARURA zipo katika hali mbaya hivyo Mkuu wa Wilaya anajukumu la kusimamia kazi zinazotekelezwa kuanzia ngazi ya kata ili kuwa na kazi bora katika jamii.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo katika kikao cha  Wakuu wa Wilaya kuhusiana na  kujenga uelewa wa majukumu ya Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini(TARURA) katika ukumbi wa Hazina Dodoma, leo.
 Baadhi ya Wakuu wa Wilaya waliohudhuria katika kikao cha kujenga uelewa wa majukumu ya Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini kilichofanyika katika ukumbi wa Hazina Dodoma, leo.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA


Hivyo makala WAZIRI JAFO: Wakuu wa Wilaya Simamieni kazi zinazofanywa na TARURA

yaani makala yote WAZIRI JAFO: Wakuu wa Wilaya Simamieni kazi zinazofanywa na TARURA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala WAZIRI JAFO: Wakuu wa Wilaya Simamieni kazi zinazofanywa na TARURA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/12/waziri-jafo-wakuu-wa-wilaya-simamieni.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "WAZIRI JAFO: Wakuu wa Wilaya Simamieni kazi zinazofanywa na TARURA"

Post a Comment

Loading...