Loading...
title : RAIS MAGUFULI AMPA POLE KANGI LUGOLA KWA KUFIWA NA MKEWE
link : RAIS MAGUFULI AMPA POLE KANGI LUGOLA KWA KUFIWA NA MKEWE
RAIS MAGUFULI AMPA POLE KANGI LUGOLA KWA KUFIWA NA MKEWE
*Lugola atoa ratiba ya maziko ya mkewe,
kuagwa Dar, kuzikwa Mwibara
Na Said Mwishehe, Blogu ya Jamii
RAIS Dk.John Magufuli ametia saini Kitabu cha Maombolezo na kumpa pole, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu Muungano na Mazingira Kangi Alphaxd Lugola aliyefiwa na mkewe Kamishina Msaidizi wa Polisi Mary Lugola.
Kamishna Mary amefariki dunia jana asubuhi akiwa katika Hospitali ya Rabinisia jijini Dar es Salaam ambako alikuwa amelazwa akipatiwa matibabu.
Rais Dk.Magufuli alifika nyumbani kwa Kangi Lugola Gerezani Railway jijini Dar es Salaam ambako ndiko msiba ulipo. Akiwa msibani Rais Magufuli ametia saini kitabu cha maombolezo na kumpa pole Lugola kwa kufiwa na mkewe Kamishna Msaidizi wa Polisi Mary Lugola.
Wakati huohuo, akizungumza na Michuzi blog kwa njia ya simu leo,Kangi Lugola amesema mkewe anatarajiwa kuagwa Januari 4 mwaka huu, kuanzia saa nne asubuhi nyumbani kwake Gerezani.
Amesema mwili utawasili nyumbani kutokea Hospitali ya Lugalo asubuhi na kisha waombolezaji wataaga mwili. Saa nane mchana mwili utasafirishawa kuelekea kijijini Mwibara mkoani Mara kwa ajili ya mazishi yatakayofanyika Januari 5 mwaka huu.
"Tunatarajia kuaga mwili wa marehemu mke wangu January 4 mwaka huu, na ikifika saa nane mchana tutausafirisha kwenda Mwibara,"amesema Kangi Lugola.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimfariji Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Kangi Lugola kwenye msiba wa mkewe MarehemuKamishna Msaidizi wa Polisi Mary Lugola Gerezani Railyways Club jijinio Dar es salaam leo January 2, 2018 .Picha na Ikulu.
Hivyo makala RAIS MAGUFULI AMPA POLE KANGI LUGOLA KWA KUFIWA NA MKEWE
yaani makala yote RAIS MAGUFULI AMPA POLE KANGI LUGOLA KWA KUFIWA NA MKEWE Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala RAIS MAGUFULI AMPA POLE KANGI LUGOLA KWA KUFIWA NA MKEWE mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/01/rais-magufuli-ampa-pole-kangi-lugola.html
0 Response to "RAIS MAGUFULI AMPA POLE KANGI LUGOLA KWA KUFIWA NA MKEWE"
Post a Comment