Loading...
title : Rasimu ya Katiba Mchezo wa Ngumi ya kabidhiwa kwa Waziri Mwakyembe
link : Rasimu ya Katiba Mchezo wa Ngumi ya kabidhiwa kwa Waziri Mwakyembe
Rasimu ya Katiba Mchezo wa Ngumi ya kabidhiwa kwa Waziri Mwakyembe
Na Anitha Jonas – WHUSM-Dar es Salaam
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe ameipongeza Kamati iliyoandaa rasimu ya katiba ya mchezo wa ngumi nchini kwa kumaliza kazi hiyo kwa wakati.
Mheshimiwa Mwakyembe ametoa kauli hiyo alipokuwa akikabidhiwa rasimu ya katiba hiyo jana jijini Dar es Salaam mara baada kukamilika kwa kuandaliwa kwake na kamati maalum iliyokuwa na wajumbe 13 wakuteuliwa ambao walifanya kazi ya kuzunguka kwa wadau wa ngumi na kukusanya maoni.
“Nitateuwa watu wasaba kutoka katika kamati hii iliyounda rasimu watakao uungana na Baraza la Michezo la Taifa kuboresha rasimu hii ili tuweze kuitisha kikao kikubwa cha wadau wote wa mchezo wa ngumi na tuweze kuipitisha rasimu hii,”Dkt.Mwakyembe.
Akiendelea kuzungumza katika makabidhiano hayo Waziri Mwakyembe alieleza kuwa ataendelea kupokea maoni ya wadau hao ndani ya miezi mitatu kwa kuzingatia sheria ili kufanikisha kikao cha kupitisha rasimu hiyo ambacho kitaitishwa kwa mujibu wa sheria ili kufanikisha lengo la kuboresha sekta ya mchezo wa ngumi nchini.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe (kushoto) akizungumza na wadau wa ngumi (hawapo pichani) kuhusu mchakato wa kukamilisha rasimu ya katiba ya kusimamia mchezo wa ngumi nchini maara baada ya kukabidhiwa jana jijini Dar es Salaam,kulia kwake ni Msajili wa Vyama vya Michezo Nchini kutoka Baraza la Michezo la Taifa Bw. Ibrahim Mkwawa.
Katibu Mtendaji Baraza la Michezo la Taifa Bw.Mohamed Kiganja (kulia) akitoa taarifa kuhusu mchakato wa kuundwa kwa rasimu ya katiba ya mchezo wa ngumi kwa Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe (kushoto) kabla ya makabidhiano ya rasimu hiyo jana jijini Dar es Salaam,wapili kulia ni Msajili wa Vyama vya Michezo Nchini kutoka Baraza la Michezo la Taifa Bw Ibrahim Mkwawa.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kuunda rasimu ya Katiba ya kusimamia mchezo wa Ngumi nchini Bw.Emmanuel Salehe akikabidhi rasimu ya katiba hiyo kwa Mheshimiwa Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe () jana jijini Dar es Salaam katikati ni Katibu Mtendaji Baraza la Michezo la Taifa Bw.Mohamed Kiganja.
Hivyo makala Rasimu ya Katiba Mchezo wa Ngumi ya kabidhiwa kwa Waziri Mwakyembe
yaani makala yote Rasimu ya Katiba Mchezo wa Ngumi ya kabidhiwa kwa Waziri Mwakyembe Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Rasimu ya Katiba Mchezo wa Ngumi ya kabidhiwa kwa Waziri Mwakyembe mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/02/rasimu-ya-katiba-mchezo-wa-ngumi-ya.html
0 Response to "Rasimu ya Katiba Mchezo wa Ngumi ya kabidhiwa kwa Waziri Mwakyembe"
Post a Comment