Loading...
title : TIBA MTANDAO KUBORESHA HUDUMA ZA AFYA NCHINI
link : TIBA MTANDAO KUBORESHA HUDUMA ZA AFYA NCHINI
TIBA MTANDAO KUBORESHA HUDUMA ZA AFYA NCHINI
Serikali imejipanga kutumia tiba mtandao kuboresha huduma za afya nchini kwenye hospitali zote za ngazi ya taifa, rufaa na wilaya ili kuwawezesha wagonjwa waishio sehemu mbali mbali nchini kupata huduma za afya kwa wakati na kwa ufanisi.
Hayo yameelezwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Mpoki Ulisubisya wakati akifungua kongamano la ubunifu na utekelezaji wa huduma za tiba mtandao Tanzania lililofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa jengo la LAPF, Dodoma.
Dkt. Ulisubisya amesema kuwa lengo la kongamano hilo ni kuwakutanisha watendaji wakuu wa hospitali za taifa nchini, madaktari bingwa wa sekta ya Afya, wakuu wa taasisi zinazoshughulika na sekta ya Afya, Wizara ya TAMISEMI, Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano; taasisi nyingine za Serikali; sekta binafsi na wabia wa maendeleo ili kujadiliana na kuwa na uelewa wa pamoja wa kufanikisha utekelezaji wa huduma za tiba mtandao ili kuboresha huduma za afya nchini.
Amesema kuwa tiba mtandao itawezesha na kuongeza ufanisi katika kufanya uchunguzi, utoaji wa tiba na madawa kwa wagonjwa wanaosumbuliwa na magonjwa mbalimbali yasiyoambukiza na yanayotokana na ajali za barabarani. “Hadi hivi sasa ni asilimia 37 tu ya wagonjwa wa kifua kikuu ndio wanaotambulika na kupatiwa huduma na Wizara ya Afya katika hospitali mbalimbali nchini. Hivyo, tiba mtandao itawezesha upatikanaji wa wagonjwa na ufikishaji wa huduma kwao kwa wagonjwa wengine asilimia 63”, amefafanua Dkt. Ulisubisya.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya akisisitiza jambo kwa wataalamu wa sekta ya afya wakati wa kongamano la ubunifu na utekelezaji wa huduma za tiba mtandao Tanzania lililofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa LAPF, Dodoma.
Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) Eng. Peter Ulanga, akiwasilisha mada kuhusu umuhimu wa tiba mtandao nchini kwa wataalamu wa sekta ya afya (hawapo pichani) wakati wa kongamano la ubunifu na utekelezaji wa huduma za tiba mtandao Tanzania ambalo limeandaliwa na UCSAF lililofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa LAPF, Dodoma.
Kaimu Mkurugenzi wa TEHAMA, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Eng. Peter Phillip Mwasalyanda (aliyeketi katikati), akisikiliza kwa makini kongamano la ubunifu na utekelezaji wa huduma za tiba mtandao Tanzania ambalo limeandaliwa na UCSAF lililofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa LAPF, Dodoma
Wataalamu wa sekta ya afya wakifuatilia kwa makini maelekezo ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Dkt. Mpoki Ulisubisya (hayupo pichani) wakati wa kongamano la ubunifu na utekelezaji wa huduma za tiba mtandao Tanzania ambalo limeandaliwa na UCSAF lililofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa LAPF, Dodoma
Hivyo makala TIBA MTANDAO KUBORESHA HUDUMA ZA AFYA NCHINI
yaani makala yote TIBA MTANDAO KUBORESHA HUDUMA ZA AFYA NCHINI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala TIBA MTANDAO KUBORESHA HUDUMA ZA AFYA NCHINI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/02/tiba-mtandao-kuboresha-huduma-za-afya.html
0 Response to "TIBA MTANDAO KUBORESHA HUDUMA ZA AFYA NCHINI"
Post a Comment