Loading...
title : MGALU AWATAADHARISHA WAKANDARASI/WATUMISHI WANAOHAMASISHA MAANDAMANO
link : MGALU AWATAADHARISHA WAKANDARASI/WATUMISHI WANAOHAMASISHA MAANDAMANO
MGALU AWATAADHARISHA WAKANDARASI/WATUMISHI WANAOHAMASISHA MAANDAMANO
Na Mwamvua Mwinyi, Kibaha
SERIKALI imetoa tahadhari kwa watumishi ,wakandarasi na wadau wa sekta ya Nishati wanao husika na miradi wasitikise kiberiti kwa kuhamasisha maandamano kupitia shida za wananchi.
Aidha wizara ya Nishati imesema itatumia kiasi cha shilingi trilioni sita kwa ajili ya kuyafikia maeneo 7,873 nchi nzima ili yaunganishwe na huduma ya umeme kupitia miradi ya Wakala wa Umeme Vijijini (REA).
Hayo yalisemwa kwenye mtaa wa Sagale Magengeni kata ya Viziwaziwa na Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu alipokuwa akitembelea maeneo yaliyoko kwenye miradi ya Wakala wa Umeme Vijijini (REA).
Alisema kuwa ole wake anayetumia tumia shida za wananchi kuhamasisha maandamano kwani akibainika chamoto atakiona.Mgalu alieleza hayo baada ya kauli ya mwananchi mmoja ambaye alikuwa akitaka umeme na kuambiwa kama anataka umeme aandamane maandamano ya Mange Kimambi.
“Serikali imeshtushwa tena inatokea maeneo haya kwa watu waliopewa dhamana mkandarasi ni dhamana huwezi kuleta jeuri kama unazo fedha usingeomba kazi hizi ni fedha za Rais Dk. Magufuli usilete jeuri,” alisema Mgalu.
Mbunge wa jimbo la Kibaha Mjini ,Silvestry Koka na Naibu waziri wa nishati Subira Mgalu wakibonyeza kiwashio ikiwa ni sehemu ya kuuwasha umeme umeme mtaa wa Mbwawa Mkoleni,wilayani Kibaha.Picha na Mwamvua Mwinyi.
Hivyo makala MGALU AWATAADHARISHA WAKANDARASI/WATUMISHI WANAOHAMASISHA MAANDAMANO
yaani makala yote MGALU AWATAADHARISHA WAKANDARASI/WATUMISHI WANAOHAMASISHA MAANDAMANO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MGALU AWATAADHARISHA WAKANDARASI/WATUMISHI WANAOHAMASISHA MAANDAMANO mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/03/mgalu-awataadharisha.html
0 Response to "MGALU AWATAADHARISHA WAKANDARASI/WATUMISHI WANAOHAMASISHA MAANDAMANO"
Post a Comment