Loading...
title : SERIKALI YAONGEZA HUDUMA ZA MATIBABU YA UGONJWA WA FIGO.
link : SERIKALI YAONGEZA HUDUMA ZA MATIBABU YA UGONJWA WA FIGO.
SERIKALI YAONGEZA HUDUMA ZA MATIBABU YA UGONJWA WA FIGO.
Na WAMJW. Dar Es salaam.
SERIKALI kupitia Wizara wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto imeongeza wigo wa kutoa huduma za matibabu ya ugonjwa wa figo nchini kwa kuongeza vituo vya usafishaji damu hadi kufikia vituo zaidi ya 17, na kufanya mafunzo kwa madaktari bingwa ili kuongezea nguvu madaktari bingwa 13 waliopo.
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt.Faustine Ndugulile wakati wa matembezi ya Siku ya figo duniani ambayo yamefanyika mapema leo katika viwanja vya Farasi Oysterbay jijini Dar es salaam.
“Wataalamu tunao 13 kwa upande wa madaktari, tumeiona hiyo changamoto kama Serikali, tumeongeza wigo wakufanya mafunzo kwa madaktari bingwa, na hivi karibuni tutatangaza ufadhili kupitia Serikali, vile vile tumetenga fedha kwaajili ya kuwafundisha madaktari ili kuweza kufanya matibabu ya figo” alisema Dkt. Ndugulile.
Dkt. Ndugulile aliendelea kusema kwamba Serikali imeongeza wigo wa usafishaji damu kwa kuongeza vituo Zaidi ya 17 ambavyo vinatoa huduma ya kusafisha damu kwa wagonjwa wa Figo katika hospitali binafsi na Hospitali za Serikali.
“Tumeongeza wigo wa usafishaji damu hadi tunavyoongea, tunavituo Zaidi ya 17 ambavyo vinatoa huduma ya kusafisha damu katika hospitali binafsi pamoja na hospitali zetu za Serikali , Muhimbili kuna vitanda 42, Mloganzira kuna vitanda 12, Bugando vitanda 6, KCMC vitanda 6, Mbeya vitanda 6, bila kusahau Regency, TMJ, Agakhan, Hindumandal, na tunaendelea kuimarisha huduma”. Alisema Dkt. Ndugulile.
Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt.Faustine Ndugulile akikata utepe kuashiria ufunguzi wa matembezi ya Siku ya figo duniani ambayo huazimishwa kila machi 8, ambayo yamefanyika katika viwanja vya Farasi Oysterbay jijini Dar es salaam
Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt.Faustine Ndugulile katika matembezi ya Siku ya figo duniani ambayo yamefanyika leo katika viwanja vya Farasi Oysterbay jijini Dar es salaam, kulia kwake ni Mwenyekiti wa Madaktari Bingwa wa Figo Dkt. Onesmo Kisanga.
Kiongozi wa Lions International Club Sayed Rizwan Qadri akikabidhi hundi ya shilingi Milioni 1.4 kwa Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt.Faustine Ndugulile ikiwa moja ya juhudi za kuunga mkono kupambana dhidi ya magonjwa ya Figo. Wakwanza kulia ni Mwenyekiti wa Madaktari Bingwa wa Figo Dkt. Onesmo Kisanga.
Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt.Faustine Ndugulile akifanya mazoezi ya viungo wakati wa kujiandaa kuanza kwa matembezi ya Siku ya figo duniani ambayo yamefanyika katika viwanja vya Farasi Oysterbay jijini Dar es salaam.
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala SERIKALI YAONGEZA HUDUMA ZA MATIBABU YA UGONJWA WA FIGO.
yaani makala yote SERIKALI YAONGEZA HUDUMA ZA MATIBABU YA UGONJWA WA FIGO. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala SERIKALI YAONGEZA HUDUMA ZA MATIBABU YA UGONJWA WA FIGO. mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/03/serikali-yaongeza-huduma-za-matibabu-ya.html
0 Response to "SERIKALI YAONGEZA HUDUMA ZA MATIBABU YA UGONJWA WA FIGO."
Post a Comment