Loading...
title : AfDB YAAHIDI KULING'ARISHA JIJI LA DODOMA NA KUONGEZA MABILIONI YA DOLA KUCHOCHEA MAENDELEO YA TANZANIA
link : AfDB YAAHIDI KULING'ARISHA JIJI LA DODOMA NA KUONGEZA MABILIONI YA DOLA KUCHOCHEA MAENDELEO YA TANZANIA
AfDB YAAHIDI KULING'ARISHA JIJI LA DODOMA NA KUONGEZA MABILIONI YA DOLA KUCHOCHEA MAENDELEO YA TANZANIA
Na Benny Mwaipaja, WFM, Dodoma
Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika-AfDB, Dkt. Akinumwi Adesina, amemaliza ziara yake ya siku tatu nchini na kuahidi kuwa atahakikisha Tanzania inaendelea kunufaika na misaada na mikopo yenye masharti nafuu kutoka Benki hiyo kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya kisasa katika Jiji la Dodoma na mradi wa kuzalisha umeme wa Stieglers Gorge.
Akiwa katika uwanja wa ndege Jijini Dodoma, Dkt. Adesina amemmwagia sifa Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa namna anavyosimamia ukuaji wa uchumi uliofikia wastani wa asilimia 7 kwa mwaka pamoja na kupambana na vitendo vya ufisadi, rushwa, kuimarisha uwajibikaji wa viongozi kwa wananchi, kupiga vita matumizi mabaya ya rasilimali za umma ili kuwaondoa wananchi wake katika umasikini.
Dkt. Adesina amesema kwa kutambua mchango huo pamoja na umahili wa Waziri wa Fedfha na mipango Dkt. Philip Mpango, wa kusimamia uchumi na sera ya bajeti na fedha, benki yake itaendelea kuwekeza kiasi kikubwa cha fedha ili nchi iweze kupiga hatua kubwa kupitia miundombinu mbalimbali inayotekelezwa kupitia benki yake na washirika wengine wa maendeleo.
Miongoni mwa miradi ambayo Benki hiyo imepanga kusaidia ni ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa utakaojengwa katika eneo la Msalato, nje kidogo ya Jiji la Dodoma ambapo kwa kuanzia benki hiyo itatoa zaidi ya shilingi bilioni 200.
“Tumekuwa na majadiliano ya kina na Mhe. Rais Dkt. John Magufuli kuhusu mradi wa kuzalisha umeme wa Stieglers Gorge ambao utazalisha Kw 2100, Benki yetu itaangalia namna ya kutoa fedha kwa ajili ya kuchangia ujenzi wa mradi huo mkubwa” alisema Dkt. Adesina.
Hivyo makala AfDB YAAHIDI KULING'ARISHA JIJI LA DODOMA NA KUONGEZA MABILIONI YA DOLA KUCHOCHEA MAENDELEO YA TANZANIA
yaani makala yote AfDB YAAHIDI KULING'ARISHA JIJI LA DODOMA NA KUONGEZA MABILIONI YA DOLA KUCHOCHEA MAENDELEO YA TANZANIA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala AfDB YAAHIDI KULING'ARISHA JIJI LA DODOMA NA KUONGEZA MABILIONI YA DOLA KUCHOCHEA MAENDELEO YA TANZANIA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/04/afdb-yaahidi-kulingarisha-jiji-la.html
0 Response to "AfDB YAAHIDI KULING'ARISHA JIJI LA DODOMA NA KUONGEZA MABILIONI YA DOLA KUCHOCHEA MAENDELEO YA TANZANIA"
Post a Comment