Loading...
title : NI LIVERPOOL AU AS ROMA KUFUZU FAINALI YA LIGI YA MABINGWA BARANI ULAYA (UEFA CHAMPIONS LEAGUE)
link : NI LIVERPOOL AU AS ROMA KUFUZU FAINALI YA LIGI YA MABINGWA BARANI ULAYA (UEFA CHAMPIONS LEAGUE)
NI LIVERPOOL AU AS ROMA KUFUZU FAINALI YA LIGI YA MABINGWA BARANI ULAYA (UEFA CHAMPIONS LEAGUE)
Na Bakari Madjeshi, Globu ya Jamii
Mchezo wa Mkondo wa pili wa Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya kati ya Liverpool ya Uingereza dhidi ya AS Roma ya Italia unatarajiwa kupigwa leo katika dimba la Uwanja wa Stadio Olimpico mjini Rome nchini Italia.
Liverpool ilishinda bao 5 - 2 katika mchezo wa mkondo wa kwanza uliopigwa Anfield, Roma wataitaji ushindi ule ule walioupata kwenye mchezo wao dhidi FC Barcelona wa bao 3 - 0 katika Robo Fainali ya Michuano hiyo ya Ulaya, ili kufika Fainali pale mjini Kiev, nchini Ukraine.
Ushindi walioupata dhidi ya Chievo Verona, Jumamosi bado unawapa moyo wa kuindosha Liverpool na kufuzu Fainali ya UEFA msimu wa 2017 – 2018.
Liverpool Mabingwa mara ya Tano Michuano ya Ulaya – ni Mafundi wa Mashambulizi ya Kushtukiza (Counterattack) hivyo Roma wanahitaji kucheza mchezo wakushambulia na kuzuia kwa umakini kutafuta magoli.
AS ROMA, wana Wachezaji wao tegemezi, Kiungo Diego Perotti ambaye anasumbuliwa na Kifundo cha Mguu (ankle), Kevin Strootman (rib) wote huenda wakakosekana katika mchezo huo baada ya kuumia katika mchezo wa mkondo wa kwanza. Beki Rick Karsdorp na Mshambuliaji , Gregoire Defrel huenda wakapewa Fatiki.
Kwa upande wa Liverpool, Kiungo Mshambuliaji wa timu hiyo, Adam Lallana amejumuishwa katika Kikosi cha Wachezaji 23 futuatia kusumbuliwa na maumivu ya Nyama za Paja (Hamstring Injury).
Nyota huyo wa Kimataifa wa Uingereza amesafiri na timu hadi Italia ijapokuwa anaonekana hayupo vizuri tangu kutolewa nje katika mchezo dhidi ya Crystal Palace mwezi March.
Lallana alisafirishwa Afrika ya Kusini kwa matibabu mwezi uliopita na Kocha Mkuu wa Liverpool amesema Wiki iliypita kwamba “Mchezo mmoja au miwili huenda akawa vizuri”, lakini hakuna nafasi ya yeye kucheza mchezo dhiidi ya Roma, siku ya leo.
chanzo: Yahoo Sports
Hivyo makala NI LIVERPOOL AU AS ROMA KUFUZU FAINALI YA LIGI YA MABINGWA BARANI ULAYA (UEFA CHAMPIONS LEAGUE)
yaani makala yote NI LIVERPOOL AU AS ROMA KUFUZU FAINALI YA LIGI YA MABINGWA BARANI ULAYA (UEFA CHAMPIONS LEAGUE) Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala NI LIVERPOOL AU AS ROMA KUFUZU FAINALI YA LIGI YA MABINGWA BARANI ULAYA (UEFA CHAMPIONS LEAGUE) mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/05/ni-liverpool-au-as-roma-kufuzu-fainali.html
0 Response to "NI LIVERPOOL AU AS ROMA KUFUZU FAINALI YA LIGI YA MABINGWA BARANI ULAYA (UEFA CHAMPIONS LEAGUE)"
Post a Comment