Loading...
title : WAZIRI WA AFYA ZANZIBAR AFANYA ZIARA YA KUTEMBELEA KITUO CHA AFYA RAHALEO NA MAKAAZI YA MADAKTARI WA CHINA NA CUBA
link : WAZIRI WA AFYA ZANZIBAR AFANYA ZIARA YA KUTEMBELEA KITUO CHA AFYA RAHALEO NA MAKAAZI YA MADAKTARI WA CHINA NA CUBA
WAZIRI WA AFYA ZANZIBAR AFANYA ZIARA YA KUTEMBELEA KITUO CHA AFYA RAHALEO NA MAKAAZI YA MADAKTARI WA CHINA NA CUBA
MUUGUZI wa Kitu cha Afya Rahaleo Wanu Amour akimuonyesha kichupa cha chanjo ya watoto Waziri wa Afya Hamad Rashid Mohamed (mwenye suti) alipofanya ziara ya kutembelea kituo hicho .
Na Ramadhani Ali – Maelezo Zanzibar.
Waziri wa Afya Hamad Rashid Mohamed amesisitiza msimamo wake wa kufuatilia na kupambana na Wafanyakazi wakorofi wenye tabia ya kuwatolea lugha chafu wagonjwa wanapofika vituo vya afya kutafuta huduma.
Amesema Wafanyakazi wengi wa vituo vya afya ni wazuri na wanatekeleza wajibu wao kwa uadilifu mkubwa lakini bado wapo wafanyakazi wachache wenye tabia ya kuwanyanyasa wagonjwa na kuwaharibia sifa nzuri wenzao. Waziri Hamad Rashid ameeleza hayo alipokuwa akizungumza na Wafanyakazi wa Kituo cha afya cha Rahaleo baada ya kufanya ziara ya ghafla katika kituo hicho.
Aliwakumbusha wafanyakazi wa sekta ya afya kuwa kilio kikubwa cha Wananchi kilikuwa ni upungufu wa dawa na lugha mbaya kwa wagonjwa lakini tatizo la dawa Serikali imelipatia ufumbuzi. Aliwataka wafanyakazi wa afya kubadilika na kuwafanyia wema na kuwapa upendo wananchi wanapofika katika vituo vyao kwa vile lugha nzuri inawapa nafuu wagonjwa .
WAZIRI wa Afya Hamad Rashid Mohamed akizungumza na Madaktari wa Kichina wanaofanya kazi Zanzibar alipotembelea Makaazi yao Mtaaa wa Vuga Mjini Zanzibar.
Hata hivyo Waziri wa Afya amewataka wagonjwa na jamaa za wagonjwa wanapofika vituo vya afya kufuata taratibu zilizowekwa ili kujenga maelewano mazuri na wafanyakazi. Aidha Waziri Hamad Rashid ameziagiza Manispaa na Mabaraza ya Miji kuimarisha usafi katika vituo vya afya kufuatia uamuzi wa Serikali wa kufanya ugatuzi na vituo hivyo kuwa chini yao.
Mfanyakazi wa Maabara wa Kituo cha Rahaleo Ineneni Fadhil Abdalla alimueleza Waziri Hamad kuwa baadhi ya wananachi wanaopeleka wagonjwa vituo vya afya wamekuwa chanzo kikubwa cha kuvuruga uhusiano mwema baina yao na wagonjwa. Amewashauri wananchi kwa upande wao kuwa wavumilivu na kuwasaidia wanapofika kupatiwa huduma ili kazi zao ziwe nyepesi zaidi.
KIONGOZI wa Madaktari kutoka Cuba Dkt. Katia Duany Baderas akizungumza na Waziri wa Afya Hamad Rashid Mohamed (alievaa suti) alipotembelea katika Makaazi yao Vuga (kulia) Naibu Waziri wa Afya Harusi Said Suleiman na wapili (kushoto) Mkurugenzi Utumishi Wizara ya Afya Ramadhani Khamis Juma .
Wakati huo huo Waziri wa Afya alitembelea makaazi ya Madaktari wa China na Cuba katika mtaa wa Vuga na kuwashukuru kwa kazi nzuri wanayofanya ya kuwahudumia wananchi wa Zanzibar. Alitoa pongezi maalum kwa Serikali ya Cuba kwa msaada mkubwa uliopelekea kuanzishwa shahada ya kwanza katika Chuo cha Taaluma za Sayansi za afya na kukubali kuwapokea wanafunzi wanaochuka shahada hiyo kwa masomo zaidi katika nchi yao.
Amewaomba wahadhiri wa Cuba wanaofundisha Chuo hicho kutoa ushauri kwa Wizara ya afya juu ya kuimarisha huduma ya afya ya msingi na mbinu zitakaosaidia kupunguza idadi ya wagonjwa wa Zanzibar wanaopelekwa nje kwa ajili ya matibabu.
DAKTARI dhamana wa Kituo cha Afya cha Rahaleo Ashura Miraji Mpatani akizungumzia changamoto na mafanikio ya Kituo cha Afya cha Rahaleo wakati wa ziara ya Waziri wa Afya Hamad Rashid (hayupo pichani).
WAZIRI wa Afya Zanzibar Hamad Rashid Mohamed akizungumza na Wafanyakazi wa Kituo cha Afya Rahaleo wakati wa ziara yake katika Kituo hicho. PICHA NA ABDALLA OMAR
Hivyo makala WAZIRI WA AFYA ZANZIBAR AFANYA ZIARA YA KUTEMBELEA KITUO CHA AFYA RAHALEO NA MAKAAZI YA MADAKTARI WA CHINA NA CUBA
yaani makala yote WAZIRI WA AFYA ZANZIBAR AFANYA ZIARA YA KUTEMBELEA KITUO CHA AFYA RAHALEO NA MAKAAZI YA MADAKTARI WA CHINA NA CUBA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WAZIRI WA AFYA ZANZIBAR AFANYA ZIARA YA KUTEMBELEA KITUO CHA AFYA RAHALEO NA MAKAAZI YA MADAKTARI WA CHINA NA CUBA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/05/waziri-wa-afya-zanzibar-afanya-ziara-ya.html
0 Response to "WAZIRI WA AFYA ZANZIBAR AFANYA ZIARA YA KUTEMBELEA KITUO CHA AFYA RAHALEO NA MAKAAZI YA MADAKTARI WA CHINA NA CUBA"
Post a Comment