Loading...
title : Ecobank yafungua tawi jipya jijini Mwanza
link : Ecobank yafungua tawi jipya jijini Mwanza
Ecobank yafungua tawi jipya jijini Mwanza

Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Mkuu wa Mkoa Mwanza John Mongella amefungua tawi jipya la Ecobank Jijini Mwanza ambapo amesema benki hiyo ina nafasi kubwa ya kuchangia ukuaji wa uchumi kupitia viwanda kwa wakazi wa Kanda ya Ziwa.
Amesema mikoa ya Kanda ya Ziwa ina utajiri mkubwa wa mazao, madini pamoja na viwanda hivyo benki hiyo inapaswa kushirikiana na wananchi kuchangia maendeleo ya viwanda kupitia huduma zake.
Aidha amesema mkoa wa Mwanza una fursa nyingi za uwekezaji ukiwa ni mkoa wa pili baada ya Dar es salaam kwa kuchangia pato la taifa hivyo miaka michache ijayo Mwanza itakuwa mshindani mkubwa kiuchumi na mkoa wa Dar es salaam ambapo tayari Mamlaka ya Bandari nchini inajiandaa kujenga bandari kavu katika eneo la Fella wilayani Misungwi hatua itakayosaidia uchumi wa mkoa kukua kwa kasi.
Mkurugenzi Mkuu Ecobank Tanzania, Mwanahiba Mzee amewahimiza wananchi wa Mwanza na Kanda ya Ziwa kwa ujumla kujiunga na benki hiyo ili kufurahia huduma zake ambapo ina matawi saba nchini, matano Jijini Dar es salaam na mawili Arusha na Mwanza huku ikiwa na ATM mashine zenye uwezo wa kupokea VISA, Master Card, China Union, Union Pay pamoja na Pan African Card.
Awali Ecobank tawi la Mwanza lilikuwa barabara ya Karuta na sasa limehamishiwa barabara ya Kenyatta jirani na mzunguko wa samaki Jijini Mwanza ambapo Mwenyekiti wa bodi ya benki hiyo nchini Peter Machunde amesema maamuzi hayo yamelenga kuboresha huduma, kuongeza ufanisi pamoja na kuwa karibu zaidi na wateja.




BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI
Hivyo makala Ecobank yafungua tawi jipya jijini Mwanza
yaani makala yote Ecobank yafungua tawi jipya jijini Mwanza Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Ecobank yafungua tawi jipya jijini Mwanza mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/06/ecobank-yafungua-tawi-jipya-jijini.html
0 Response to "Ecobank yafungua tawi jipya jijini Mwanza"
Post a Comment