Loading...
title : MAKAMU WA RAIS AWASILI IGUNGA MKOANI TABORA
link : MAKAMU WA RAIS AWASILI IGUNGA MKOANI TABORA
MAKAMU WA RAIS AWASILI IGUNGA MKOANI TABORA
Mheshimiwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo ameanza ziara ya kikazi katika Mkoa wa Tabora ambapo atatembelea Wilaya zote saba (7) za Igunga, Nzega, Uyui, Sikonge, Kaliua, Urambo na Tabora .
Lengo la ziara ni kutembelea miradi mbalimbali ya maendeleo ili kujionea utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya mwaka 2015 ya Chama Cha Mapinduzi, kuhamasisha wananchi kushiriki shughuli za maendeleo na kutoa maelekezo kwa watendaji kuhusu masuala mbalimbali ya kiutendaji yatakayobainika katika ziara.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Tabora Mzee Hassan Wakasubi mara baada ya kuwasili Igunga, katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Aggrey Mwanri. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akivishwa skafu na kijana wa skauti mara baada ya kuwasili Igunga mkoani Tabora. (picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Hivyo makala MAKAMU WA RAIS AWASILI IGUNGA MKOANI TABORA
yaani makala yote MAKAMU WA RAIS AWASILI IGUNGA MKOANI TABORA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MAKAMU WA RAIS AWASILI IGUNGA MKOANI TABORA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/02/makamu-wa-rais-awasili-igunga-mkoani.html
0 Response to "MAKAMU WA RAIS AWASILI IGUNGA MKOANI TABORA"
Post a Comment