Loading...

Muogeleaji Natalia atamba kushinda mashindano ya kuogelea ya Marekani

Loading...
Muogeleaji Natalia atamba kushinda mashindano ya kuogelea ya Marekani - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Muogeleaji Natalia atamba kushinda mashindano ya kuogelea ya Marekani, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Muogeleaji Natalia atamba kushinda mashindano ya kuogelea ya Marekani
link : Muogeleaji Natalia atamba kushinda mashindano ya kuogelea ya Marekani

soma pia


Muogeleaji Natalia atamba kushinda mashindano ya kuogelea ya Marekani

Dar es Salaam. Muogeleaji wa Tanzania, Natalia Ladha ametamba kufanya vyema katika mashindano ya kuogelea ya kutafuta tiketi ya kufuzu kwa mashindano ya Olimpiki ya jimbo la Florida nchini Marekani yajulikanayo kwa jina la Florida Gold Coast Junior Olympic.

Natalia aliondoka nchini jana tayari kwa mashindano hayo yaliyopangwa kufanyika Martin County Juni 16 ambapo atajiunga na waogeleaji wa klabu ya Swimfast.

Muogeleaji huyo ambaye ni nyota kwa waogeleaji wa Tanzania wenye umri kati ya miaka tisa na 10, anashindana katika mashindano hayo makubwa matano Marekani kwa mara ya pili mfulilizo.

“Nimejiandaa vizuri kwa ajili ya mashindano hayo na natarajia kufanya vyema kwa waogeleaji wenye umri kama wangu, nimejiandaa vyema katika nikiwa na makocha wangu wa klabu ya Taliss,” alisema Natalia.

Katika mashindano yam waka jana ya Miami, Natalia alishinda medali ya shaba kwa mita 50 na 100 kwa upande wa staili ya backstroke.

Natalia pia alitamba katika mashindano ya staili nyingine ambapo alitwaa medali ya dhahabu kwa mita 200 freestyle, 200 ( individual medley), 100m (backstroke),50m (butterfly) na medali ya fedha kwa mita 100 katika staili ya butterfly. Pia alishinda medali ya dhahabu kwa mita 100 katika freestyle.

Mbali ya mashindano hayo, Natalia pia atashiriki katika mashindano ya umri ya Coral Spring ambayo yataanza Juni 15 na kumalizika Juni 17 na vile vile mashindano ya Fort Lauderdale yaliyopangwa kuanza Juni 22 mpaka 24.

Vile vile atashiriki katika mashindano ya Sectionals, yaliyopangwa kuanza Julai 6 mpaka 9 ma Area championships yaliyopangwa kuanza Julai 13 mpaka 15, mjini Sunrise.


Hivyo makala Muogeleaji Natalia atamba kushinda mashindano ya kuogelea ya Marekani

yaani makala yote Muogeleaji Natalia atamba kushinda mashindano ya kuogelea ya Marekani Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Muogeleaji Natalia atamba kushinda mashindano ya kuogelea ya Marekani mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/06/muogeleaji-natalia-atamba-kushinda.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "Muogeleaji Natalia atamba kushinda mashindano ya kuogelea ya Marekani"

Post a Comment

Loading...