Loading...
title : MAKAMU WA RAIS AHUDHURIA UFUNGUZI MKUTANO WA 31 WA WAKUU WA NCHI NA SERIKALI WA UMOJA WA AFRIKA NCHINI MAURITANIA
link : MAKAMU WA RAIS AHUDHURIA UFUNGUZI MKUTANO WA 31 WA WAKUU WA NCHI NA SERIKALI WA UMOJA WA AFRIKA NCHINI MAURITANIA
MAKAMU WA RAIS AHUDHURIA UFUNGUZI MKUTANO WA 31 WA WAKUU WA NCHI NA SERIKALI WA UMOJA WA AFRIKA NCHINI MAURITANIA
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu leo amehudhuria ufunguzi wa Mkutano wa 31 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika (AU) katika mji Nouakchott, Mauritania.
Pamoja na mambo mengine mkutano huu umejikita katika masuala ya Kupambana na Rushwa katika bara la Afrika, Mkakati wa Biashara ya Pamoja ,masuala ya Ulinzi na Amani katika nchi za Congo DRC, Burundi na Sahara Magharibi, pamoja na kujadili masuala ya mabadiliko yatakayoleta tija katika Utawala na kuboresha uchumi.
Makamu wa Rais anamuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli. Katika hotuba ya Ufunguzi wa mkutano huo, Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika ,Rais wa Rwanda Paul Kagame alisema “ Kama umoja, tupo pamoja na watu Ethiopia na Zimbabwe, kufuatia mabadiliko ya kisiasa ya amani. Tunashutumu mashambulizi yaliotaka kuvuruga amani na tunatoa pole kwa waliopoteza maisha”.
Kagame amesema pia wameridhiswa na hatua zinazoendelea za kuleta Amani Sudani ya Kusini. Mkutano huo unatarajiwa kumalizika kesho ambapo kuna uwezekano mkubwa Viongozi hawa wa Afrika watakutana na Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron wakati wa chakula cha mchana .
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akijadiliana jambo na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Augustine pamoja na Viongozi waandamizi wakati ufunguzi wa Mkutano wa 31 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika (AU) katika mji Nouakchott, Mauritania Makamu wa Rais anamuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli katika mkutano huo. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akifuatilia kwa makini yanayoendelea kwenye ufunguzi wa Mkutano wa 31 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika (AU) katika mji Nouakchott, Mauritania ambako anamuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais).Picha zaidi: Makamu wa Rais ahudhuria ufunguzi wa Mkutano wa AU Mauritania.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akifuatilia kwa makini yanayoendelea kwenye ufunguzi wa Mkutano wa 31 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika (AU) katika mji Nouakchott, Mauritania ambako anamuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais).Picha zaidi: Makamu wa Rais ahudhuria ufunguzi wa Mkutano wa AU Mauritania.
Hivyo makala MAKAMU WA RAIS AHUDHURIA UFUNGUZI MKUTANO WA 31 WA WAKUU WA NCHI NA SERIKALI WA UMOJA WA AFRIKA NCHINI MAURITANIA
yaani makala yote MAKAMU WA RAIS AHUDHURIA UFUNGUZI MKUTANO WA 31 WA WAKUU WA NCHI NA SERIKALI WA UMOJA WA AFRIKA NCHINI MAURITANIA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MAKAMU WA RAIS AHUDHURIA UFUNGUZI MKUTANO WA 31 WA WAKUU WA NCHI NA SERIKALI WA UMOJA WA AFRIKA NCHINI MAURITANIA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/07/makamu-wa-rais-ahudhuria-ufunguzi.html
0 Response to "MAKAMU WA RAIS AHUDHURIA UFUNGUZI MKUTANO WA 31 WA WAKUU WA NCHI NA SERIKALI WA UMOJA WA AFRIKA NCHINI MAURITANIA"
Post a Comment