Loading...
title : MADIWANI WATANO PWANI WAKIMBILIA CCM LEO NI PAMOJA NA RAMADHANI LUTAMBI WA KATA YA MAILMOJA
link : MADIWANI WATANO PWANI WAKIMBILIA CCM LEO NI PAMOJA NA RAMADHANI LUTAMBI WA KATA YA MAILMOJA
MADIWANI WATANO PWANI WAKIMBILIA CCM LEO NI PAMOJA NA RAMADHANI LUTAMBI WA KATA YA MAILMOJA
MADIWANI watano wa vyama vya upinzani ikiwemo Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA, CUF na ACT Mzalendo na viongozi wengine sita wamevikimbia vyama hivyo na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoani Pwani.
Madiwani hao ni pamoja na Ramadhan Lutambi aliyekuwa diwani wa kata ya Mailmoja kupitia Chadema na Ramadhan Kombe aliyekuwa diwani kata Mbwawa kupitia ACT.
Wengine ni, Muharami Mkopi Cuf kata ya Ruaruke wilayani Kibiti,Seif Lwambo kupitia Cuf kata ya Beta,Muharami Mketo Cuf Kata ya Lukanga na Mwenyekiti wa Kijiji cha Lukanga.
Aidha viongozi waliojiuzulu kwenye vyama hivyo ni Ayubu Chapile ambae alikuwa katibu kata ya Mkuza (CUF) ,Karimu Kasimu katibu tawi chuo kikuu cha Mwalimu Nyerere (Chadema) ,Selemani Mwinyimkuu mwenyekiti tawi (Cuf),David Mramba Act,Latifa Sangalala mwanachama Chadema Mkoani B na Jumanne Urembo Diwani kivuli ACT kata ya Sofu.
Awali Ramadhani Lutambi alisema ,chama kinachofaa kuongoza nchi daima ni CCM kwani vyama vingine havina uwezo,na havijali viongozi wa ngazi za chini .
Alifafanua ,ameamua kuondoka Chadema ili kutekeleza yale yanayofanywa na Rais Dk. Magufuli kwa wananchi wanyonge.
Lutambi alikiri kuondoka Chadema kwa hiari yake, kwa akili zake timamu na kudai anajivua vyeo vyote alivyonavyo kuanzia sasa.
Aliyekuwa diwani wa kata ya Mailmoja, Kibaha Ramadhani Lutambi kupitia Chama Cha Chadema amekimbilia Chama Cha Mapinduzi (CCM)
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoani Pwani Ramadhani Maneno akizungumza baada ya kuwapokea madiwani watano kutoka upinzani na viongozi na wanachama wengine wa vyama hivyo wapatao sita.

Aliyekuwa diwani wa kata ya Mailmoja, Kibaha Ramadhani Lutambi kupitia Chama Cha Chadema akiwapungia mkono baadhi ya wananchi na wanachama wa CCM katika ofisi za CCM mkoani Pwani baada ya kuacha chama hicho na kukimbilia Chama Cha Mapinduzi (CCM) (picha na Mwamvua Mwinyi)
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala MADIWANI WATANO PWANI WAKIMBILIA CCM LEO NI PAMOJA NA RAMADHANI LUTAMBI WA KATA YA MAILMOJA
yaani makala yote MADIWANI WATANO PWANI WAKIMBILIA CCM LEO NI PAMOJA NA RAMADHANI LUTAMBI WA KATA YA MAILMOJA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MADIWANI WATANO PWANI WAKIMBILIA CCM LEO NI PAMOJA NA RAMADHANI LUTAMBI WA KATA YA MAILMOJA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/08/madiwani-watano-pwani-wakimbilia-ccm.html
0 Response to "MADIWANI WATANO PWANI WAKIMBILIA CCM LEO NI PAMOJA NA RAMADHANI LUTAMBI WA KATA YA MAILMOJA"
Post a Comment