Loading...

RC BRIGEDIA JENERALI MWANGELA AKATAA OMBI LA MKANDARASI KUONGEZEWA MUDA

Loading...
RC BRIGEDIA JENERALI MWANGELA AKATAA OMBI LA MKANDARASI KUONGEZEWA MUDA - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa RC BRIGEDIA JENERALI MWANGELA AKATAA OMBI LA MKANDARASI KUONGEZEWA MUDA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : RC BRIGEDIA JENERALI MWANGELA AKATAA OMBI LA MKANDARASI KUONGEZEWA MUDA
link : RC BRIGEDIA JENERALI MWANGELA AKATAA OMBI LA MKANDARASI KUONGEZEWA MUDA

soma pia


RC BRIGEDIA JENERALI MWANGELA AKATAA OMBI LA MKANDARASI KUONGEZEWA MUDA

Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brigedia Jenerali Nicodemas E Mwangela akikagua ujenzi wa daraja la Kikamba linalounganisha kata ya Kapalala na Gua Wilayani Songwe, katika ziara yake ya siku mbili wilayani humo aliyoianza leo. Daraja hilo limeanza kujengwa Oktoba 20, 2017 na linatarajiwa kukamilika Septemba, 2018 likiwa limegharimu shilingi bilioni 1.4.
Ujenzi wa daraja la Kikamba linalounganisha kata ya Kapalala na Gua Wilayani Songwe ukiendelea, Daraja hilo limeanza kujengwa 20 Oktoba, 2017 na linatarajiwa kukamilika Septemba, 2018 likiwa limegharimu shilingi bilioni 1.4.

Na Grace Gwamagobe, Songwe

Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brigedia Jenerali Nicodemas E Mwangela amekataa ombi la Mkandarasi kutoka kampuni ya Mats Engineering Ltd Paulo Philipo Paulo la kuongezewa kipindi cha miezi miwili ili aweze kukamilisha ujezi wa Daraja la Kikamba Wilayani Songwe.

Brigedia Jenerali Mwangela amekataa ombi hilo leo alipokagua ujenzi wa daraja la Kikamba linalounganisha kata za Kapalala na Gua wilayani Songwe kwakuwa sababu alizotoa mkandarasi huyo hazijitosheleji.

Amesema daraja hilo lazima likamilike kwa muda uliopangwa ambao ni Septemba, 2018 huku mkandarasi huyo akitoa sababu kuwa atachelewa kukamilisha ujenzi huo kutokana na mvua nyingi zilizonyesha na mwamba mgumu uliopo eneo la ujenzi.

“Mkandarasi ahakikishe anafanya kazi mchana na usiku ili akamilishe ndani ya muda wa mkataba, vifaa vya kumuwezesha kufanya hivyo anavyo na ombi la kuongezewa muda wa ujenzi mimi siafikiani nalo”, amesema Brigedia Jenerali Mwangela.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Songwe Samuel Jeremia amesema yeye na viongozi wengine wataendelea kusimamia miradi ya maendeleo na katika ujenzi wa daraja hilo watahakikisha wanamsimamia mkandarasi huyo ili amalize ndani ya muda uliopangwa.

Daraja la Kikamba linaolunganisha kata za Kapalala na Gua limeanza kujengwa mwezi Oktoba 2017 na linatarajiwa kukamilia Septemba 2018 likiwa limegharimu shilingi bilioni 1.4.


Hivyo makala RC BRIGEDIA JENERALI MWANGELA AKATAA OMBI LA MKANDARASI KUONGEZEWA MUDA

yaani makala yote RC BRIGEDIA JENERALI MWANGELA AKATAA OMBI LA MKANDARASI KUONGEZEWA MUDA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala RC BRIGEDIA JENERALI MWANGELA AKATAA OMBI LA MKANDARASI KUONGEZEWA MUDA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/08/rc-brigedia-jenerali-mwangela-akataa.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "RC BRIGEDIA JENERALI MWANGELA AKATAA OMBI LA MKANDARASI KUONGEZEWA MUDA"

Post a Comment

Loading...