Loading...

WACHEZAJI 11 WAONDOLEWA CECAFA U17

Loading...
WACHEZAJI 11 WAONDOLEWA CECAFA U17 - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa WACHEZAJI 11 WAONDOLEWA CECAFA U17, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : WACHEZAJI 11 WAONDOLEWA CECAFA U17
link : WACHEZAJI 11 WAONDOLEWA CECAFA U17

soma pia


WACHEZAJI 11 WAONDOLEWA CECAFA U17


Wachezaji wawili wa timu ya taifa ya vijana ya Tanzania chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Boys, Jafar Mtoo na Lenox Fred Chande ni miongoni mwa wachezaji 11 walioondolewa kwenye michuano ya kuwania kushiriki Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa vijana wa umri huo (Afcon U17) wa Afrika Mashariki na Kati baada ya kuzidi umri.
Wachezaji hao wameondolewa baada ya zoezi la vipimo vya kuthibitisha umri (MRI) lililofanyika hospitali ya Muhimbili na kusimamiwa na madaktari wa Shirikisho la Soka Afrika (Caf) kwa ajili ya michuano hiyo ijulikanayo kama Cecafa Caf Afcon qualifier ambayo ilianza jana Dar es Salaam.
Wachezaji walioondolewa walikutwa wamezidi umri wa miaka 17 katika vipimo vya madaktari wa Caf iliyobadili mfumo wa mashindano ya kufuzu kwa Afcon U17 ni Yacine Zerquin kutoka Algeria na Sherif Ahmed wa Misri.
Taarifa ya Makamu wa Rais wa Kamati ya Tiba ya Caf, Dk Yacine Zerguini imewataja wachezaji wengine walioenguliwa ni Abdoul Intwari wa Burundi, Maxwell Mullili, Lesley Otieno na Abdulmalik Hussein Abdallah wa Kenya, Simon Pitia Alberto wa Sudan Kusini, Gamel Abdou Kamal wa Sudan, Oluka George, Kafumbe Joseph na Elvis Ngonde wa Uganda.
Michuano ya kufuzu ya Cecafa Afcon ilianza inaanza jana kwenye Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam kwa mchezo kati ya Rwanda na Sudan Saa 8:00 kabla ya wenyeji, Tanzania kumenyana na Burundi Saa 11:00 jioni. Bingwa wa mashindano atafuzu moja kwa moja kwa Afcon U17 ya mwakani, ambayo Tanzania ni mwenyeji na tayari imekata tiketi hiyo kutokana na uenyeji huo.chanzo :habari leo.


Hivyo makala WACHEZAJI 11 WAONDOLEWA CECAFA U17

yaani makala yote WACHEZAJI 11 WAONDOLEWA CECAFA U17 Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala WACHEZAJI 11 WAONDOLEWA CECAFA U17 mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/08/wachezaji-11-waondolewa-cecafa-u17.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "WACHEZAJI 11 WAONDOLEWA CECAFA U17"

Post a Comment

Loading...