Loading...
title : Airtel Tanzania yatoa msaada kwa kituo cha yatima Morogoro
link : Airtel Tanzania yatoa msaada kwa kituo cha yatima Morogoro
Airtel Tanzania yatoa msaada kwa kituo cha yatima Morogoro
Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania kupitia kitengo chake cha huduma kwa wateja imetoa msaada wa vitu mbali mbali kwa kituo cha yatima cha Mgolole Orphanage Center, Morogoro.
Msaada huo ni pamoja na vitanda, neti, magodoro, deep freezer, chupa za chai, hot pot, sukari, sahani, sabuni, nepi, pampers na toy za watoto vyote vikiwa na thamani ya TZS 18 milioni.
Kutoa kwa msaada huo ni muendeleo wa kampuni ya Airtel Tanzania kupitia programu ya Airtel Tunakujali ambapo wafanyakazi wa kampuni hiyo kukubali kutoa sehemu ya mshahara wao ili kusaidi huduma za kijamii na hasa kwa watoto wanaoishi katika mazingira magumu.
Akiongea mara baada ya kutoa msaada huo kwa kituo hicho cha Mgolole cha Morogoro, Mkurugenzi wa Kitengo cha Huduma kwa Wateja Airtel Tanzania Adriana Lyamba alisema muda mrefu wafanya kazi wa Airtel kupitia Airtel tunakujali imekuwa ikitembelea na kusaidia vituo mbali mbali vya yatima ikiwa ni pamoja na kuwapa misaada mbali mbali.
Leo ni siku yenye furaha sana kwetu zote kwani mayatima ni sehemu ya Jamii yetu na ni muhimu kuwapa upendo pamoja na kuwafariji. Hiki ambacho tumekuja kutoa leo hapa ni kidogo lakini nina uhakika kitagusa mioyo yenu lakini zaidi ni kujua tuko pamoja nanyi na tunawajali sana, alisema Lyamba.
Naomba kutoa pongezi za dhati kwa wafanyakazi wenzangu wa Airtel kwa kukubali kutoa sehemu ya kipato chao na leo tumeweza kufika hapa. Lakini zaidi napongeza uongozi wa kampuni yetu kwa kukubali na kuridhia programu yetu hii hapa ya Airtel Tunakujali ambayo imekuwa ikituleta karibu na Jamii inayotuzunguka, alisema Lyamba.
Tunayo furaha kuweza kuwafikia watoto hawa ambao wako kwenye kituo hiki na dhamira yetu ni kuendelea kugusa maisha ya watoto wanaoishi kwenye mazingira mangumu na kuwafanya wajisikia kuwa sehemu ya familia ya Airtel, aliongeza Lyamba.
Kwa upande wake, Makamu Mama Mkuu wa kituo cha Mgolole Sista Valeria Mnyanzaga alisema ni furaha kwa kampuni kubwa ya Airtel kuguzwa na maisha ya watoto wanaoishi kwenye kituo hiki na hatimaye kuja kutoa msaada na kutuunga mkono.
Mkurugenzi wa Kitengo cha Huduma kwa Wateja Airtel Tanzania Adriana Lyamba (kulia) akikabidhi msaada kwa Makamu Mama Mkuu wa kituo cha yatima cha Mgolole, Morogoro. Airtel Tanzania kupitia mradi wake wa Airtel Tunakujali walitembelea kituo hicho pamoja na kutoa msaada wa vitu mbalimbali vyenye dhamani ya TZS 18 milioni mwishoni mwa wiki.
Mkurugenzi wa Kitengo cha Huduma kwa Wateja Airtel Tanzania Adriana Lyamba (kulia) akikabidhi msaada wa dogoro kwa Makamu Mama Mkuu wa kituo cha yatima cha Mgolole, Morogoro. Airtel Tanzania kupitia mradi wake wa Airtel Tunakujali walitembelea kituo hicho pamoja na kutoa msaada wa vitu mbali mbali vyenye dhamani ya TZS 18 milioni mwishoni mwa wiki. Kati kati ni Meneja wa Kitengo cha huduma kwa wateja Airtel Tanzania Deogratius Hugo.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala Airtel Tanzania yatoa msaada kwa kituo cha yatima Morogoro
yaani makala yote Airtel Tanzania yatoa msaada kwa kituo cha yatima Morogoro Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Airtel Tanzania yatoa msaada kwa kituo cha yatima Morogoro mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/10/airtel-tanzania-yatoa-msaada-kwa-kituo.html
0 Response to "Airtel Tanzania yatoa msaada kwa kituo cha yatima Morogoro"
Post a Comment