Loading...
title : Makamu wa rais atembelea mradi wa ujenzi wa tenki la maji la Bagamoyo leo
link : Makamu wa rais atembelea mradi wa ujenzi wa tenki la maji la Bagamoyo leo
Makamu wa rais atembelea mradi wa ujenzi wa tenki la maji la Bagamoyo leo
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Hassan Suluhu ametembelea mradi wa ujenzi wa tenki la maji la Bagamoyo lililojengwa na Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es salaam (DAWASA).
Mama Samia akiwa katika ziara ya siku tano Mkoa wa Pwani kuanzia Oktoba 24 hadi 29 atatembelea miradi mbalimbali ikiwemo mradi wa Kisarawe ulio chini ya Mamlaka hiyo.
Akielezea mradi huo kwa Makamu wa Rais, Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja amesema kuwa mradi huu ni msaada kutoka benki ya Exim unaotarajiwa kukamilika Desemba Mwaka huu.
Kwenye mradi huo wa Bagamoyo, Mama Samia ametembelea ujenzi wa tenki lenye uwezo wa kuhifadhi maji Lita Milioni 6 kwa siku likiwa ni moja kati ya mradi wa uboreshaji wa huduma za ugawaji na usambazaji maji katika baadhi ya maeneo ya Mkoa wa Pwani.
Mradi huo unaotekelezwa na Wizara ya Maji na Umwagiliaji kupitia Mamlaka ya Majisafi na Majitaka (DAWASA) ulianza rasmi mwezi Machi mwaka 2016 na utakamilika 2018.
Kazi zinazofanyika chini ya mradi huu na katika mfumo unaohudumiwa na Mtambo wa Ruvu Chini ni pamoja na ujenzi wa matenki tisa ya kuhifadhi na kusambaza maji yenye ukubwa wa kuhifadhi lita Milioni 3.0 hadi 6.0.
Mbali na mradi wa matenki, kuna ujenzi wa vituo vinne vya kusukumia maji, ununuzi wa transfoma na ufungaji wa umeme wa msongo Mkubwa, ununuzi na ulazaji wa mabomba makubwa ya ugawaji maji na ulazaji wa mabomba ya usambazaji maji mitaani yatakayokuwa na urefu wa jumla ya Kilometa zipatazo 80.
Utekelezaji wa mradi huo kwa sasa unaendelea vizuri na mwaka huu wananchi wa maeneo yatakayopita mradi wa Bagamoyo wameanza kufaidika.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Hassan akizungumza mara baada alipotembelea mradi wa maji wa Bagamoyo unaotekelezwa na Mamlaka Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA) chini ya Wizara ya Maji na Umwagiliaji wakati alipotembelea ujenzi wa tenki la maji lenye uwezo wa kuhifadhi maji lita Milioni sita kwa siku.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA) Mhandisi Cyprian Luhemeja akzungumza wakati Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Hassan alipotembelea mradi wa maji wa Bagamoyo unaotekelezwa na Mamlaka hiyo chini ya Wizara ya Maji na Umwagiliaji wakati alipotembelea ujenzi wa tenki la maji lenye uwezo wa kuhifadhi maji lita Milioni sita kwa siku.

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA) Mhandisi Cyprian Luhemeja akimuelezea Makamu ww Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Hassan Suluhu mradi wa maji wa Bagamoyo unaotekelezwa na Mamlaka hiyo chini ya Wizara ya Maji na Umwagiliaji wakati alipotembelea ujenzi wa tenki la maji lenye uwezo wa kuhifadhi maji Lita Milion sita kwa siku.
Hivyo makala Makamu wa rais atembelea mradi wa ujenzi wa tenki la maji la Bagamoyo leo
yaani makala yote Makamu wa rais atembelea mradi wa ujenzi wa tenki la maji la Bagamoyo leo Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Makamu wa rais atembelea mradi wa ujenzi wa tenki la maji la Bagamoyo leo mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/10/makamu-wa-rais-atembelea-mradi-wa.html
0 Response to "Makamu wa rais atembelea mradi wa ujenzi wa tenki la maji la Bagamoyo leo"
Post a Comment