Loading...

Mkuu wa Mkoa ahimiza stahiki za wafanyakazi

Loading...
Mkuu wa Mkoa ahimiza stahiki za wafanyakazi - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Mkuu wa Mkoa ahimiza stahiki za wafanyakazi, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Mkuu wa Mkoa ahimiza stahiki za wafanyakazi
link : Mkuu wa Mkoa ahimiza stahiki za wafanyakazi

soma pia


Mkuu wa Mkoa ahimiza stahiki za wafanyakazi

Abraham Ntambara

Saidi Meck Sadik
MKUU wa Mkoa wa Kilimanjaro, Saidi Meck Sadik, amewataka waajiri kutekeleza wajibu wao wa kuwapa wafanyakazi stahiki zao kwa mujibu wa kanuni na taratibu za kazi.

Kauli hiyo aliitoa jana wakati akitoa salamu za mkoa huo katika maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani ambayo kitaifa yalifanyika mkoani humo.

“Waajiri wanatakiwa kutenda haki kwa wafanyakazi. Wanatakiwa kuwapa wafanyakazi stahiki zao kwa maana hiyo wanatakiwa kutekeleza wajibu wao huo,” alisema Sadik.

Alibainisha kuwa katika mkoa huo wafanyakazi wamekuwa wakifanya kazi kwa ufanisi kutokana na kufahamu vema falasafa ya Serikali, akisema hiyo inathibitika kutokana na kutoendekeza maandamano.

Mkuu wa Mkoa alimwomba Rais John Magufuli asaidie kuhakikisha viwanda ambavyo havifanyi kazi mkoani humo vinafufuka ili kuongeza ajira kwa vijana.

Alieleza kuwa Kilimanjaro ilikuwa na viwanda vingi vilivyokuwa vikitoa ajira nyingi kwa wananchi, lakini sasa havifanyi kazi na kubainisha kuwa vipo ambavyo viliuzwa, lakini hadi leo havifanyi kazi.

“Suala la viwanda mkoani Kilimanjaro, wewe (Rais) ni shahidi, Moshi kulikuwa na viwanda vingi, vilikuwa vinatoa ajira zaidi ya 10,000, vyote vimekufa, vijana wanazurura bila ajira,” alisema Sadik.

Alisema kwa kuwa Rais amedhamiria kufufua viwanda, ni vema asimamie suala hilo ili vianze uzalishaji na vijengwe vingine vipya ili kuondoa tatizo la ajira.

Aidha, aliwataka wakazi wa mkoa huo kujenga viwanda mkoani kwao kwa kuwa wana fedha za kutosha badala ya kujenga mikoa mingine ambako alieleza kufanya hivyo kutasaidia kuleta maendeleo.



Hivyo makala Mkuu wa Mkoa ahimiza stahiki za wafanyakazi

yaani makala yote Mkuu wa Mkoa ahimiza stahiki za wafanyakazi Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Mkuu wa Mkoa ahimiza stahiki za wafanyakazi mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/05/mkuu-wa-mkoa-ahimiza-stahiki-za.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "Mkuu wa Mkoa ahimiza stahiki za wafanyakazi"

Post a Comment

Loading...