Loading...
title : SADAKA NETWORK YAWAOMBA WATANZANIA KUCHANGIA FEDHA KUFANIKISHA UPASUAJI WA WANAWAKE NA WATOTO
link : SADAKA NETWORK YAWAOMBA WATANZANIA KUCHANGIA FEDHA KUFANIKISHA UPASUAJI WA WANAWAKE NA WATOTO
SADAKA NETWORK YAWAOMBA WATANZANIA KUCHANGIA FEDHA KUFANIKISHA UPASUAJI WA WANAWAKE NA WATOTO
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
TAASISI isiyo ya kiserikali ya SADAKA Network imeunga mkono juhudi za Hospitali ya Aga Khan, Muhimbili na Taasisi ya Women to Women katika kufanikisha upasuaji wa urekebishaji (upasuaji wa urembo) kwa wanawake na watoto utakaofanyika 27 November mwaka huu.
Hospitali ya Agha Khan, Muhimbili na Taaisis ya Women to Women ziko kwenye harakati za kuweka tabasamu kwenye nyuso za wahanga wa ukatili wa nymbani uliosababisha wahanga hao kuathirika.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam, Mwanzilishi wa SADAKA Network Dkt Ibrahim Msengi amesema kuwa SADAKA Network umeamua kuunga mkono kwa kuchangisha fedha kupitia programu yake ili kufanikisha mpango huo, wameamua kutumia viongozi wa jamii na watu maarufu ndani ya Tanzania kuhabarisha wananchi wote ili waweze kuchangisha fedha ili kwa pamoja waweze kusaidia kurejesha tabasamu kwenye uso zao.
Dkt Ibrahim amesema kuwa, ukatili wa nyumbani na ajali unaweza ukasababisha mauti au majeraha yanayoweza kubadilisha muelekeo wa maisha ya yao, watu wameshuhudia, kusikia au kuona kupitia luninga wanawake na watoto ambao muonekano wao umebadilika kisa ajali au ukatili wa nyumbani au watoto wenye maisha yaliybadilishwa kisa wazazi waliowakatili.
Mwanzilishi wa SADAKA Network Dkt Ibrahim Msengi akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na taasisi yake kuunga mkono juhudi za Hospitali ya Aga Khan, Muhimbili na Taasisi ya Women to Women katika kufanikisha upasuaji wa urekebishaji (upasuaji wa urembo) kwa wanawake na watoto utakaofanyika 27 November mwaka huu, kushoto ni Shekhe Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Alhad Mussa Salum na Meneja Masoko na Mahusiano wa Agha Khan Hospital Olayce Steven Lotha .
Meneja Masoko na Mahusiano wa Agha Khan Hospital Olayce Steven Lotha akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na upasuaji wa urekebishaji (upasuaji wa urembo) kwa wanawake na watoto utakaofanyika 27 November mwaka huu.
Balozi wa Rejesha tabasamu usoni mwao Yvyone Cherry akiwa anawahisi jamii kuchangia kwa kiasi chochote ili kufanikisha upasuaji wa wanawake na watoto waliofanyika ukatili majumbani. Kushoto ni Askofu Mkuu wa Kanisa la Anglikana Jackson Jackson, Mwanzilishi wa SADAKA Network Dkt Ibrahim Msengi na Shekhe Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Alhad Mussa Salum.
Waandishi wa habari na wadau mbalimbali wakifuatilia mkutano huo.
Hivyo makala SADAKA NETWORK YAWAOMBA WATANZANIA KUCHANGIA FEDHA KUFANIKISHA UPASUAJI WA WANAWAKE NA WATOTO
yaani makala yote SADAKA NETWORK YAWAOMBA WATANZANIA KUCHANGIA FEDHA KUFANIKISHA UPASUAJI WA WANAWAKE NA WATOTO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala SADAKA NETWORK YAWAOMBA WATANZANIA KUCHANGIA FEDHA KUFANIKISHA UPASUAJI WA WANAWAKE NA WATOTO mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/11/sadaka-network-yawaomba-watanzania.html
0 Response to "SADAKA NETWORK YAWAOMBA WATANZANIA KUCHANGIA FEDHA KUFANIKISHA UPASUAJI WA WANAWAKE NA WATOTO"
Post a Comment