Loading...

WAZIRI KAIRUKI ATAKA KAGUZI ZA MARA KWA MARA MIGODIN

Loading...
WAZIRI KAIRUKI ATAKA KAGUZI ZA MARA KWA MARA MIGODIN - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa WAZIRI KAIRUKI ATAKA KAGUZI ZA MARA KWA MARA MIGODIN, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : WAZIRI KAIRUKI ATAKA KAGUZI ZA MARA KWA MARA MIGODIN
link : WAZIRI KAIRUKI ATAKA KAGUZI ZA MARA KWA MARA MIGODIN

soma pia


WAZIRI KAIRUKI ATAKA KAGUZI ZA MARA KWA MARA MIGODIN



Na Asteria Muhozya, Chunya

Waziri wa Madini Angellah Kairuki amewataka Maafisa Madini nchini kuhakikisha wanafanya kaguzi za mara kwa mara katika maeneo ya wachimbji wadogo ikiwemo kutoa elimu ya uchimbaji, masuala ya afya na usalama kazini ili kuongeza tija katika shughuli hizo.

Waziri Kairuki aliyasema hayo Novemba 27, wakati akikagua maendeleo ya ujenzi wa Kituo cha Umahiri Chunya kinachojengwa na Mkandarasi kampuni ya SUMAJKT.

Alisema, wachimbaji wadogo wanatakiwa kulelelewa ili watoke katika uchimbaji mdogo wa madini kwenda uchimbaji wa Kati na hatimaye kuwa wachimbaji wakubwa, na kueleza kuwa, ili kufikia azma hiyo elimu ya mara kwa mara kwa wachimbaji ni muhimu ikatolewa kwani itawezesha serikali kupata mapato kutokana na kufuata uchimbaji sahihi.

Pia, aliwataka Maafisa hao kuhakikisha kuwa wanatatua migogoro katika maeneo yao kwani suala hilo litawezesha uzalishaji zaidi na kupelekea serikali kunufaika na shughuli hizo, ikiwemo ongezeko la ajira na ustawi wa jamii.

Vilevile, Waziri Kairuki alieleza kuwa, pamoja na kwamba katika Mwaka wa Fedha 2018/19 wizara yake imepangiwa kukusanya shilingi bilioni 310, lakini kama anataka makusanyo hayo yafikie shilingi bilioni 500 na kuongeza kwamba, Maafisa madini watapimwa kutokana na ukusanyo huo wa maduhuli.

Waziri wa Madini Angellah Kairuki akiangalia ramani ya jengo la Kituo cha Umahiri Chunya litakavyokuwa mara baada ya kukamilika kwake. Jengo hilo linajengwa na Mkandarasi SUMAJKT. 
Waziri wa Madini Angellah Kairuki akisikiliza jambo kutoka kwa Mkandarasi SUMAJKT alipotembelea kukagua maendeleo ya ujenzi wa Kituo cha Umahiri Chunya. Wengine ni Wataalam kutoka Ofisi za Madini Mbeya na Chunya, wataalam kutoka Wizara ya Madini, na uongozi wa Wilaya ya Chunya. 
Sehemu ya jengo la Kituo cha Umahiri Chunya likiwa katika maendeleo ya ujenzi wake. 
Sehemu ya viongozi wa Wilaya, viongozi wa Ofisi za Madini Mbeya na Chunya pamoja na wadau wa madini wilayani humo wakimsikiliza Waziri wa Madini Angellah Kairuki (hayupo pichani). 



Hivyo makala WAZIRI KAIRUKI ATAKA KAGUZI ZA MARA KWA MARA MIGODIN

yaani makala yote WAZIRI KAIRUKI ATAKA KAGUZI ZA MARA KWA MARA MIGODIN Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala WAZIRI KAIRUKI ATAKA KAGUZI ZA MARA KWA MARA MIGODIN mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/11/waziri-kairuki-ataka-kaguzi-za-mara-kwa.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "WAZIRI KAIRUKI ATAKA KAGUZI ZA MARA KWA MARA MIGODIN"

Post a Comment

Loading...