Loading...

WAZIRI MKUU AZINDUA VIZA NA VIBALI VYA UKAAZI VYA KIELEKTRONIKI

Loading...
WAZIRI MKUU AZINDUA VIZA NA VIBALI VYA UKAAZI VYA KIELEKTRONIKI - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa WAZIRI MKUU AZINDUA VIZA NA VIBALI VYA UKAAZI VYA KIELEKTRONIKI, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : WAZIRI MKUU AZINDUA VIZA NA VIBALI VYA UKAAZI VYA KIELEKTRONIKI
link : WAZIRI MKUU AZINDUA VIZA NA VIBALI VYA UKAAZI VYA KIELEKTRONIKI

soma pia


WAZIRI MKUU AZINDUA VIZA NA VIBALI VYA UKAAZI VYA KIELEKTRONIKI

*Yawataka watakaopewa kufanya shughuli zilizoelekezwa kwenye vibali vyao.

WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amezindua huduma za viza na vibali vya ukaazi vya kielektroniki na amewataka watu wote watakaopewa vibali hivyo kutii sheria kwa kufanya shughuli ambazo wameelekezwa kwa mujibu wa vibali vyao na si vinginevyo.

Amesema utoaji wa huduma hizo ni miongoni mwa jitihada za Serikali katika kuvutia uwekezaji, hususan katika sekta ya viwanda kwani hatua hiyo itarahisisha upatikanaji wa vibali hivyo kwa raia wa kigeni na kuchochea kasi ya maendeleo ya kiuchumi.

Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Jumatatu, Novemba 26, 2028) wakati akizindua huduma za viza na vibali vya ukaazi vya kielektroniki katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es Salaam na kwamba hatua hiyo itasaidia kuondoa urasimu na ucheleweshwaji wa huduma pamoja na kuimarisha ulinzi na usalama wa nchi.

Amesema Idara ya Uhamiaji inatarajia kuanza kutoa huduma tajwa kwa raia wa kigeni muda wowote kuanzia sasa na kwa kupitia huduma hiyo, raia wa kigeni wataweza kuomba vibali hivyo kwa njia ya kielektroniki wakati wowote na mahali popote walipo.

Waziri Mkuu amesema watakaopewa vibali wanatakiwa kufanya shughuli zao kwa mujibu wa vibali vyao kwa sababu kufanya shughuli tofauti na ilivyoainishwa kwenye kibali ni kosa kwa mujibu wa Sheria na Kanuni za Uhamiaji. 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akizindua Viza na Vibali vya Ukaazi vya Kielektroniki  kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius  Nyerere jijini Dar es salaam, Novemba 26, 2018.  Kulia ni  Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi, Mhandisi Hamad Masauni na wapili kulia ni Kamishina Jenerali wa Idara ya Uhamiaji, Dkt. Anna Makalala.  


 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na  Kamishina Jenerali wa Idara ya Uhamiaji Nchini, Dkt. Anna Makalala wakati alipowasili kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius  Nyerere jijini Dar es salaam  Kuzindua  Viza na Vibali vya Ukaazi vya Kielektroniki , Novemba 26, 2018.  Katikati ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, Dkt. Augustine Mahiga  (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na  Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa  Nchini (TAKUKURU)  Kamishaina wa Polisi, Diwani Athumani baada ya Kuzindua Viza na Vibali vya Ukaazi vya Kielektroniki kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius  Nyerere jijini Dar es salaam, Novemba 26, 2018.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Jaji Mkuu wa Tanzania Mstaafu, Augustino Ramadhani baada ya Kuzindua Viza na Vibali vya Ukaazi vya Kielektroniki kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius  Nyerere jijini Dar es salaam, Novemba 26, 2018. 

 Baadhi  ya Washiriki wa Uzinduzi wa  Viza na Vibali vya Ukaazi vya Kielektroniki  wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza kabla ya uzinduzi huo kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es salaam , Novemba 26, 2018.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA>>>>>


Hivyo makala WAZIRI MKUU AZINDUA VIZA NA VIBALI VYA UKAAZI VYA KIELEKTRONIKI

yaani makala yote WAZIRI MKUU AZINDUA VIZA NA VIBALI VYA UKAAZI VYA KIELEKTRONIKI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala WAZIRI MKUU AZINDUA VIZA NA VIBALI VYA UKAAZI VYA KIELEKTRONIKI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/11/waziri-mkuu-azindua-viza-na-vibali-vya.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "WAZIRI MKUU AZINDUA VIZA NA VIBALI VYA UKAAZI VYA KIELEKTRONIKI"

Post a Comment

Loading...