Loading...

Naibu Waziri Shonza awapa TBC wiki moja kukamilisha ujenzi wa Kituo cha kurushia Matangazo Longido

Loading...
Naibu Waziri Shonza awapa TBC wiki moja kukamilisha ujenzi wa Kituo cha kurushia Matangazo Longido - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Naibu Waziri Shonza awapa TBC wiki moja kukamilisha ujenzi wa Kituo cha kurushia Matangazo Longido, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Naibu Waziri Shonza awapa TBC wiki moja kukamilisha ujenzi wa Kituo cha kurushia Matangazo Longido
link : Naibu Waziri Shonza awapa TBC wiki moja kukamilisha ujenzi wa Kituo cha kurushia Matangazo Longido

soma pia


Naibu Waziri Shonza awapa TBC wiki moja kukamilisha ujenzi wa Kituo cha kurushia Matangazo Longido


Na Anitha Jonas – WHUSM,Namanga -Arusha.

Naibu Waziri Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa naMichezo Mhe.Juliana Shonza ameuagiza uongozi wa Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) Kanda ya Kaskazini kukamilisha ujenzi wa kituo cha kurusha matangazo kinachojenga Makao Makuu ya Wilaya ya Longido ndani ya wiki moja.

Mheshimiwa Shonza ametoa agizo hilo leo Wilayani Longido alipotembelea kituo cha kurusha matangazo ya TBC kinachojengwa Wilayani hapo kwa lengo la kutatua kero ya kukosekana kwa usikivu wa matangazo ya TBC ambapo wananchi wa eneo hilo wamekuwa wakisikiliza radio za nchi jirani na hiyo imewafanya kukosa taarifa zenye ukweli na uhakika za ndani ya nchi.

“Chumba hichi cha kuhifadhi busta na mitambo mingine ni kidogo sana na ujenzi wake siyo wa kuchukua muda mrefu hakikisheni mpaka Januari 10,muwe mmekamilisha ujenzi wa Kituo hichi wananchi wa Longido wanakiu kubwa ya kutaka kusikia matangazo kutoka chombo hichi cha serikali chenye habari za ukweli na uhakika na hii ni haki yao,”alisema Mhe.Shonza.

Akiendelea kuzungumza katika ziara hiyo Naibu Waziri huyo aliwasisitiza viongozi hao wa TBC kuhakikisha ujenzi wa kituo hicho cha kurushia matangazo kinajengwa kwa kutumia vifaa imara kwani serikali ilitenga bajeti yenye fedha za kutosha kwa ajili ya kuhakikisha usikivu unaboreshwa katika maeneo ya mipakani na malengo ya serikali ni kabla ya mwa 2020 kero hii ya usikivu iwe imekwisha.

Naibu Waziri Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mheshimiwa Juliana Shonza (wa kwanza kulia) akitoa maelekezo ya kukamilika kwa ujenzi wa kituo cha kurushia matangazo Longido ndani ya wiki moja kwa Meneja wa Kanda ya Kaskazini Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) Bw.Gerald Uisso (hayupo pichani) alipotembelea eneo hilo leo lilopo katika ofisi za Wilaya ya Longido,(katikati) ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Longido Bw.Jumaa Mhina. 
Meneja wa TBC Kanda ya Kaskazini Bw.Gerald Uisso (wa kwanza kulia) akimwonyesha Naibu Waziri Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mheshimiwa Juliana Shonza (katikati) nyumba ambayo imejengwa kwa ajili ya kuweka busta za kurushia matangazo pamoja na mitambo leo alipotembelea eneo hilo Wilayani Longido linapojengwa mitambo hiyo kwa lengo ya kuthibiti changamoto ya usikivu wa matangazo ya TBC,wa (kwanza kushoto) ni Katibu Tawala Wilaya ya Longido Bw. Toba Nguvila. 
Naibu Waziri Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mheshimiwa Juliana Shonza (wa kwanza kushoto) akimsikiliza Fundi Mitambo wa TBC Mhandisi Christopher Mkama akitoa maelezo kuhusu hali ya usikivu kwa eneo la Namaga alipotembelea kituo hicho cha kurusha matangazo ya TBC kilichopo Namanga leo ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kufuatiliaji wa usikivu kwa Kanda ya Kaskazini . 



Hivyo makala Naibu Waziri Shonza awapa TBC wiki moja kukamilisha ujenzi wa Kituo cha kurushia Matangazo Longido

yaani makala yote Naibu Waziri Shonza awapa TBC wiki moja kukamilisha ujenzi wa Kituo cha kurushia Matangazo Longido Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Naibu Waziri Shonza awapa TBC wiki moja kukamilisha ujenzi wa Kituo cha kurushia Matangazo Longido mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/12/naibu-waziri-shonza-awapa-tbc-wiki-moja.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "Naibu Waziri Shonza awapa TBC wiki moja kukamilisha ujenzi wa Kituo cha kurushia Matangazo Longido"

Post a Comment

Loading...