Loading...

Prof. Msanjila awataka Stamico kujitangaza mtambo wa kuchoronga miamba

Loading...
Prof. Msanjila awataka Stamico kujitangaza mtambo wa kuchoronga miamba - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Prof. Msanjila awataka Stamico kujitangaza mtambo wa kuchoronga miamba, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Prof. Msanjila awataka Stamico kujitangaza mtambo wa kuchoronga miamba
link : Prof. Msanjila awataka Stamico kujitangaza mtambo wa kuchoronga miamba

soma pia


Prof. Msanjila awataka Stamico kujitangaza mtambo wa kuchoronga miamba

Na Nuru Mwasampeta, Dodoma 

Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini Prof. Simon Msanjila amelitaka Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) kutumia mtambo wa kuchoronga miamba kwa ufanisi ili kuliletea tija Taifa pamoja na shirika hilo kutokana na kipato kitakachotokana na uwepo wa mtambo huo.

Prof. Msanjila ameyasema hayo  jana desemba 24, 2018 wakati wa hafla fupi ya kuukabidhi rasmi mtambo huo kwa STAMICO kwa ajili ya kuanza kuutumia rasmi. Mtambo huo unaitwa Multi-Purpose Air Rotary Drill Rig.

Akizungumza katika makabidhiano hayo, Prof. Msanjila amesema, ununuzi wa mtambo huo ni uwekezaji mkubwa ambao Serikali imeufanya kwa shirika la Stamico hivyo, halina budi kuutumia vyema ili uweze kuleta tija.

Akizungumzia gharama za mtambo huo, Prof. Msanjila amesema umegharimu kiasi cha Dola za Kimarekani milioni moja na laki tatu(USD 1.3) ambazo yeye kama Mtendaji Mkuu wa wizara anaona kuwa na deni kubwa kwake, na hivyo kuahidi kuusimamia ipasavyo ili kuhakikisha mtambo huo unazalisha faida na kuwa chachu ya kuweza kununua mitambo mingine kama hiyo ili kukuza sekta ya madini nchini.

Aidha, amelitaka Shirika hilo kujitangaza vema ili wananchi na hususn wadau wa madini wanaojihusisha na shughuli za uchimbaji na utafutaji wa madini kufahamu uwepo wa mtambo huo ili uweze kutumika hata kwa kampuni binafsi ili kujiongezea kipato lakini pia kuwasaidia wachimbaji wadogo wa madini. “Kwa zabuni nilizozisikia mpaka sasa mtambo huu utazalisha pesa za kutosha” amesema Msanjila.

Mbali na kukabidhi mtambo huo, Prof. Msanjila ameitaka Stamico kuwasilisha taarifa za mapato na matumizi ya mtambo huo kila robo ya mwaka ili kuweza kufanya tathmini endapo mtambo unatumika kwa faida.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Prof. Simon Msanjila (Kushoto) akimkabidhi Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO Kanali Sylvester Ghuliku hati ya makabidhiano ya mtambo wa kuchoronga miamba unaojulikana kama Multi-Purpose Air Rotary Drill Rig. 
Kaimu Mkurugenzi wa Utawala na RasilimaliWatu Nsajigwa Kabigi pamoja na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO Kanali Sylvester Ghuliku wakisaini hati za makabidhiano ya mtambo wa kuchoronga miamba. 
Kaimu Mkurugenzi wa Utawala na RasilimaliWatu Nsajigwa Kabigi (Kushoto) na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO Kanali Sylvester Ghuliku wakionesha hati za makabidhiano mara baada ya kusaini. 

Mtambo wa kuchoronga miamba uliogharimu kiasi cha dola za kimarekani milioni 1.3. Mtambo huu unajulikana kama Multi-Purpose Air Rotary drill Rig. 



Hivyo makala Prof. Msanjila awataka Stamico kujitangaza mtambo wa kuchoronga miamba

yaani makala yote Prof. Msanjila awataka Stamico kujitangaza mtambo wa kuchoronga miamba Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Prof. Msanjila awataka Stamico kujitangaza mtambo wa kuchoronga miamba mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/12/prof-msanjila-awataka-stamico.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "Prof. Msanjila awataka Stamico kujitangaza mtambo wa kuchoronga miamba"

Post a Comment

Loading...