Loading...

Wajasiriamali 777 Wajengewa Uwezo na MKURABITA Singida

Loading...
Wajasiriamali 777 Wajengewa Uwezo na MKURABITA Singida - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Wajasiriamali 777 Wajengewa Uwezo na MKURABITA Singida, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Wajasiriamali 777 Wajengewa Uwezo na MKURABITA Singida
link : Wajasiriamali 777 Wajengewa Uwezo na MKURABITA Singida

soma pia


Wajasiriamali 777 Wajengewa Uwezo na MKURABITA Singida

Mwambawahabari
Na: Mwandishi Wetu
Wajasiriamali 777 wa mjini Singida wamenufaika na mafunzo yaliyoandaliwa na Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge (MKURABITA) ili kuwajengea uwezo wa kurasimisha biashara  zao na kutoa mchango stahiki katika ujenzi wa uchumi.
Akizungumza wakati akifunga mafunzo kwa wajsiriamali hao mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi amesema kuwa Dhamira ya Serikali ni kuwawezesha wajasiriamali kufanya biashara kwa tija na kuchochea maendeleo.
"Mafunzo haya yametolewa kwa namna itakayowawezesha wajasiriamali wetu hapa Singida kuwa na mfumo bora wa kufanya biashara  na kuleta mabadiliko makubwa kwa wajasiriamali"
Akifafanua amesema kuwakila majasiriamali anapaswa kuwa mwadilifu, mzalendo  na mwenye mpangilio mzuri wa namna yakuendesha biashara yake, anayethemini muda, anayetii sheria na kujali wateja anaowahudumia ili kuchochea ukuaji wa Biashara husika.
Aliongeza kuwa wananchi mkoani humo wana imani kubwa na Serikali ya Awamu ya Tano kwa kuwa inajali ustawi wa wanyonge ndio maana imeweka mkazo katika kuwawezesha kupitia mipango na pragramu mbalimbali zinazotekelezwa ikiwemo uwezeshaji kupitia MKURABITA unaolenga kuwapa ujuzi wa namna bora ya kufanya biashara.
Aidha aliwaasa wajasiriamali hao kuhakiksiha kuwa wanatumia vizuri mikopo watakayopata kutoka katika taasisi za fedha ili iweze kuwasaidia kukuza biashara zao na kufikia malengo kusudiwa ya kuanzisha biashara husika.
Aliwaasa wajasiriamali hao kuelewa dhana ya kuchukua mkopo kuwa ni kukuza na kuendeleza biashara na sivinginevyo hivyo wajiepushe na tabia ya kukopa fedha na kuzielekeza katika masuala yasiyoendana naukuzaji wa biashara zao ili kuepeka migogogro na kurudisha nyuma juhudi za kukuza biashara hapa nchini.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Urasimishaji Bw. Japhet Werema amesema kuwa wajasiriamali hao wanayo fursa yakuendelea kujengewa uwezo kupitia kituo kimoja cha huduma kinachofunguliwa katika Manispaa ya Singida ili kuendeleza kazi yakuwahudumia wajasiriamali kwa karibu zaidi ambapo taasisi zote zinzohudumia wajasiriamali zitakuwa zikitoa huduma katika eneo moja na hivyo kupunguza usumbufu kwa wajasiriamali hao.
Aliongeza kuwa dhamira ya mafunzo  hayo ni kujenga uwezo kwa wajasiriamali hao ili warasimishe biashara zao na kuzingatia taratibu za uendeshaji biashara zenye tija kwa maslahi yao na Taifa kwa ujumla ambapo wamefundishwa kuhusu  utunzaji wa kumbukumbu, umuhimu wa kodi, masuala ya hifadhi za jamii, Umuhimu wa urasimishaji biashara.
Naye Meya wa Manispaa hiyo Alhaji Gwae Chima amesema kuwa wanaipongeza MKURABITA  kwa kuwajengea uwezo wajasirimali hao ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa weledi.
Pia alipongeza Serikali ya Awamu ya Tano kwa juhudi inazochukua katika kuwawezesha wananchi hasa wanayonge kote nchini ili washiriki kikamilifu katika ujenzi wa uchumi.
Mafunzo kwa wajasiriamali hao zaidi ya 777 yamefanyika mjini Singida  yakiratibiwa na kuendeshwa na MKURABITA kwa kushirikiana na Manispaa ya Singida.


Hivyo makala Wajasiriamali 777 Wajengewa Uwezo na MKURABITA Singida

yaani makala yote Wajasiriamali 777 Wajengewa Uwezo na MKURABITA Singida Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Wajasiriamali 777 Wajengewa Uwezo na MKURABITA Singida mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/12/wajasiriamali-777-wajengewa-uwezo-na.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "Wajasiriamali 777 Wajengewa Uwezo na MKURABITA Singida"

Post a Comment

Loading...