Loading...
title : WANAFUNZI 12,399 WACHAGULIWA KIDATO CHA KWANZA MWAKA 2019 AWAMU YA KWANZA SIMIYU
link : WANAFUNZI 12,399 WACHAGULIWA KIDATO CHA KWANZA MWAKA 2019 AWAMU YA KWANZA SIMIYU
WANAFUNZI 12,399 WACHAGULIWA KIDATO CHA KWANZA MWAKA 2019 AWAMU YA KWANZA SIMIYU
Na Stella Kalinga, Simiyu
Jumla ya Wanafunzi 12,399 mkoani Simiyu wamechaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza kwa mwaka 2019 katika shule za Serikali za kutwa na bweni kwa awamu ya kwanza. Hayo yamebainishwa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini Desemba 14, 2019 wakati akitoa taarifa ya uchaguzi wa wanafunzi wa Kidato cha kwanza kwa mwaka 2019 Mjini Bariadi.
Sagini amesema jumla ya wanafunzi waliofaulu Mtihani wa Darasa la Saba ni 24,983 sawa na asilimia70.68 ya wanafunzi wote waliofanya mtihani, ambapo amebainisha kuwa wanafunzi 12, 584 kati ya 24,983 waliofaulu hawajachaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza kutokana na uhaba wa miundombinu ya elimu.
Sagini amesema lengo la Serikalini kuhakikisha wanafunzi wote waliofaulu wanaenda sekondari hivyo, amewaagiza Wakurugenzi wa Halmashauri zote mkoani Simiyu kuhakikisha kuwa wanafanya jitihada katika ujenzi na ukamilishaji wa miundombinu, ili wanafunzi wote waliofaulu mtihani wa darasa la saba waweze kuanza kidato cha kwanza kwa wakati.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini akitoa taarifa ya uchaguzi wa wanafunzi wa kidato cha kwanza mwaka 2019, Desemba 14, 2018 Mjini Bariadi.
Afisa Elimu wa Mkoa wa Simiyu, Mwl. Ernest Hinju akitoa taarifa ya hali ya ufaulu katika Mtihani wa kuhitimu darasa la saba mwaka 2018, katika kikao cha uchaguzi wa wanafunzi wa kidato cha kwanza mwaka 2019 kilichofanyika Desemba 14, 2018 Mjini Bariadi.
Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi, Mhe. Bahame Kaliwa (kushoto) na Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa,Mhe. Paul Maige wakifuatilia kwa makini nyaraka zenye taarifa ya uchaguzi wa wanafunzi wa kidato cha kwanza mwaka 2019, katika kikao kilichofanyika Desemba 14, 2018 Mjini Bariadi.
Baadhi ya wajumbe wa Kikao cha uchaguzi wa wanafunzi wa kidato cha kwanza mwaka 2019, wakimsikiliza Mwenyekiti wa Kikao hicho na Katbu Tawala Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini akifungua kikao hicho Desemba 14, 2018 Mjini Bariadi.
Baadhi ya waandishi wa habari na wajumbe wa Kikao cha uchaguzi wa wanafunzi wa kidato cha kwanza mwaka 2019, wakimsikiliza Mwenyekiti wa Kikao hicho na Katbu Tawala Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini akifungua kikao hicho Desemba 14, 2018 Mjini Bariadi.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala WANAFUNZI 12,399 WACHAGULIWA KIDATO CHA KWANZA MWAKA 2019 AWAMU YA KWANZA SIMIYU
yaani makala yote WANAFUNZI 12,399 WACHAGULIWA KIDATO CHA KWANZA MWAKA 2019 AWAMU YA KWANZA SIMIYU Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WANAFUNZI 12,399 WACHAGULIWA KIDATO CHA KWANZA MWAKA 2019 AWAMU YA KWANZA SIMIYU mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/12/wanafunzi-12399-wachaguliwa-kidato-cha.html
0 Response to "WANAFUNZI 12,399 WACHAGULIWA KIDATO CHA KWANZA MWAKA 2019 AWAMU YA KWANZA SIMIYU"
Post a Comment