Loading...
title : Naibu Katibu Mkuu UWT Taifa ampongeza Rais Magufuli kwa kutoa fedha ujenzi wa kituo cha afya Pangani
link : Naibu Katibu Mkuu UWT Taifa ampongeza Rais Magufuli kwa kutoa fedha ujenzi wa kituo cha afya Pangani
Naibu Katibu Mkuu UWT Taifa ampongeza Rais Magufuli kwa kutoa fedha ujenzi wa kituo cha afya Pangani
Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Bara kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Jesca Mbogo ametoa pongezi kwa Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa kutoa fedha za ujenzi wa Kituo cha Afya Mwera kilichopo Wilaya ya Pangani mkoani Tanga.
Mbogo alitoa pongezi hizo jana ikiwa ni siku ya pili ya ziara yake mkoani Tanga, yenye lengo la kujionea utekelezaji wa Ilani ya CCM ya mwaka 2015/20 na namna inavyogusa maisha ya akina mama.
"Namshukuru sana Rais Magufuli kwa kuboreshea Kituo hiki kwani akinamama sasa watapata huduma za afya hapa na kuepuka adha ya kusafiri umbali mrefu kwa kivuko hadi Pangani kutafuta matibabu". Alisema Mbogo ambaye ameanza ziara yake ya kwanza mkoani Tanga tangu ateuliwe kuwa Naibu Katibu Mkuu UWT Tanzania Bara.
Mbogo pia alipokea shukrani za akina mama wilayani Pangani waliomshukru Rais Magufuli kwa juhudi zake za kuboresha huduma za afya nchini ikiwemo ujenzi wa Kituo cha Afya Mwera kitakachowarahisishia upatikanaji wa huduma za afya.

Naibu Katibu Mkuu UWT Tanzania Bara, Jesca Mbogo akisaini kitabu cha wageni.

Naibu Katibu Mkuu UWT Tanzania Bara, Jesca Mbogo.

Naibu Katibu Mkuu UWT Tanzania Bara, Jesca Mbogo akizungumza na akina mama wilayani Pangani (hawako pichani).

Naibu Katibu Mkuu UWT Tanzania Bara, Jesca Mbogo akizungumza na akina mama wilayani Pangani.

Akina mama wilayani Pangani wakimsikiliza Naibu Katibu Mkuu UWT Tanzania Bara, Jesca Mbogo.

Zawadi

Naibu Katibu Mkuu UWT Tanzania Bara, Jesca Mbogo alipata fursa ya kupata mche maalumu kama ishara ya mwanzo moya wa maboresho ya huduma za afya kwa akina mama.
Hivyo makala Naibu Katibu Mkuu UWT Taifa ampongeza Rais Magufuli kwa kutoa fedha ujenzi wa kituo cha afya Pangani
yaani makala yote Naibu Katibu Mkuu UWT Taifa ampongeza Rais Magufuli kwa kutoa fedha ujenzi wa kituo cha afya Pangani Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Naibu Katibu Mkuu UWT Taifa ampongeza Rais Magufuli kwa kutoa fedha ujenzi wa kituo cha afya Pangani mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/01/naibu-katibu-mkuu-uwt-taifa-ampongeza.html
0 Response to "Naibu Katibu Mkuu UWT Taifa ampongeza Rais Magufuli kwa kutoa fedha ujenzi wa kituo cha afya Pangani"
Post a Comment