Loading...
title : Waziri Ummy: ifikapo mwaka 2020 katika wagonjwa 100 wa Kifua Kikuu tutawaibua 70 na kuwapatia matibabu
link : Waziri Ummy: ifikapo mwaka 2020 katika wagonjwa 100 wa Kifua Kikuu tutawaibua 70 na kuwapatia matibabu
Waziri Ummy: ifikapo mwaka 2020 katika wagonjwa 100 wa Kifua Kikuu tutawaibua 70 na kuwapatia matibabu
Hussein Ndubikile
Mwamba wa Habari
Serikali imesema ifikapo mwaka 2020 imejiwekea mikakati kuhakikisha katika kila wagonjwa 100 wa Kifua Kikuu inawaibua wagonjwa 70 na kuwapa matibabu huku ikibainisha takwimu za kiduania mwaka jana zinaonyesha watu 154,000 kila mwaka huugua ugonjwa huo.
Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu kabla ya Hafla ya kukabidhi Magari 10 na Pikipiki 35 ambazo zimekabidhiwa kwa Waratibu Halmashauri na Waganga wa Mikoa kwa ajili ya kupambana na ugonjwa wa Kifua Kifuu na Ukoma.
Amesema kuwa Tanzania katika mapambano ya ugonjwa imeonyesha nia ya dhati na kwamba mwaka 2020 watahakikisha kati ya wagonjwa 100 wa ugonjwa huo wanafikiwa na kupewa tiba.
“ Mgonjwa wa kifua kikuu asipoptaiwa tiba ana uwezo wa kuambukiza watu 20 kila mwaka hadi tumefanikiwa kupunguza ugonjwa kwa asilimia 44 huku asilimia 56 wako katika nyumba, vijiji, mtaani na maofisini,” amesema waziri Ummy.
Amebainisha kuwa kwa asilimia 85 Serikali inatumia vifaa vya sampuli za kutolea majibu ya ugonjwa huo ndani ya saa mbili na kwamba katika wagonjwa 100, wagonjwa 90 wanatumia dawa.
Amesisitiza kuwa magari na pikipiki hizo zitacahangia kuongeza nguvu kwa waratibu na waganga katika mapambano ya ugonjwa huo.
Waziri Ummy amesema kuna wagonjwa 2000 wa ugonjwa wa ukoma katika halmashauri za Liwale, Nkasi, Kilombero, Mvomero, Nachingwea, Pangani na Korogwe.
Amewataka wakuu wa shule za bweni za Serikali na Binafsi kuacha kupokea wanafunzi ambao hawana fomu za matokeo ya ugonjwa wa kifua kikuu na kuwaagiza waganga wa mikoa kwenda kufanya ukaguzi wa fomu za wanafunzi.
Ameitaja miongoni mwa mikoa iliyokabidhiwa magari ni Pwani, Ilala, Songwe, Kilimanjaro, Tabora na Rukwa.
Halmashauri zilizokabidhiwa pikipiki ni Ngara, Urambo, Nzega, Ujiji, Mbulu, Hanang, Msalala, Kilolo, Amana, Mbagala, Mburahati, Tanga, Muheza, Kilombero na Gairo
Kwa upande wake Mwakilishi Mkazi wa Shirika lisilo la Kiserikali la Ujerumani-Tanzani linalojishughulisha na mapambano dhidi ya ugonjwa wa Kifua Kikuu na Ukoma (GLRA), Burchard Rwamtoga amesema asasi hiyo ilianza kazi ya kusaidia wagonjwa huo na ukoma mwaka 1959 na kupata usajili mwaka 1977.
Amesema asasi hiyo hushirikiana kwa miaka mitano mitano na serikali na kwamba makubaliano ya sasa ni kuanzia mwaka 2015 hadi 2020.
Burchard amebainisha katika kipindi cha miaka 21 wamesaidia Mpango wa Kudhibiti Kifua Kikuu na Ukoma magri 270 kwa waratibu wa mikoa na pikpiki 675 kwa waratibu wa mikoa.
Pia amesema mwaka 2018 GLRA limesaidia kununua magari 9 aina ya Toyota Landcruiser Hard Top, gari moja Suzuki Jimny na Pikpiki 35 aina ya Honda XL 125.
Ametaja gharama za magari 9 ni Sh 661,370,760 bila uhuru huku Suzuki Jimny ni Sh 30,485,000/- bila ushuru huku akibainisha Pikipiki 35 zimegharimu Sh 221,047,016 (bila ushuru).
Katika hatua nyingine amesema magari 10 yaliyokabidhiwa yote yamekatiwa bima kubwa kwa kipindi cha mwaka mmoja.
Hivyo makala Waziri Ummy: ifikapo mwaka 2020 katika wagonjwa 100 wa Kifua Kikuu tutawaibua 70 na kuwapatia matibabu
yaani makala yote Waziri Ummy: ifikapo mwaka 2020 katika wagonjwa 100 wa Kifua Kikuu tutawaibua 70 na kuwapatia matibabu Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Waziri Ummy: ifikapo mwaka 2020 katika wagonjwa 100 wa Kifua Kikuu tutawaibua 70 na kuwapatia matibabu mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/01/waziri-ummy-ifikapo-mwaka-2020-katika.html
0 Response to "Waziri Ummy: ifikapo mwaka 2020 katika wagonjwa 100 wa Kifua Kikuu tutawaibua 70 na kuwapatia matibabu"
Post a Comment