Loading...

MBINU MPYA YA KUSAFIRISHA DAWA ZA KULEVYA YABAINIKA

Loading...
MBINU MPYA YA KUSAFIRISHA DAWA ZA KULEVYA YABAINIKA - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa MBINU MPYA YA KUSAFIRISHA DAWA ZA KULEVYA YABAINIKA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : MBINU MPYA YA KUSAFIRISHA DAWA ZA KULEVYA YABAINIKA
link : MBINU MPYA YA KUSAFIRISHA DAWA ZA KULEVYA YABAINIKA

soma pia


MBINU MPYA YA KUSAFIRISHA DAWA ZA KULEVYA YABAINIKA

Dixon Busagaga, Globu ya Jamii - Moshi

WAFANYABIASHARA  wa Dawa za kulevya aina ya Mirungi wamebuni mbinu mpya za kusafirisha Dawa hizo kwa kutumia magari ya Kifahari yakiwemo Toyota Land Cruser ,Toyota Alphasad,Toyota Vanguard huku wengine wakilazimka kuzifanyia mabadiliko gari aina ya Toyota Noah ili kurahisisha ubebaji wa Mirungi kwa kificho.

Hata hivyo tayari jeshi la Polisi mkoa wa Kilimanjaro limebaini mbinu hizo baada ya kufanikiwa kukamata gari aina ya Toyota Noah lenye namba za usajili T 443 DET lililokuwa limebeba kilogramu 102 za Mirungi likielekea Kondoa mkoani Dodoma.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro ,Kamishna Msaidizi wa Polisi ,Hamis Issah alithibitisha kukamatwa kwa gari hilo majira ya saa 6:30 za usiku katika kizuizi cha askari eneo la Kwa Wasomali likielekea njia ya Arusha.

“Tumeendelea na zoezi la kukamata wasafirishaji w Dawa za kulevya ,tumekamata kwa mara nyingine gari aina ya Noah ,hili gari limetokea maeneo ya mkoani Kilimanjaro ,linaelekea mkoani Dodoma katika wilaya ya Kondoa “alisema Kamanda Issah.
“Hili gari limebadilishwa badilishwa ndani  ,ukilitizama limejengewa vyumba maeneo tofauti tofauti kwa ajili ya kuekea Mirungi,Bampa la mbele lina vyumba ,ndani kumetobolewa na kuchomelewa vizuri ,yaani limefanyiwa mabadiliko makubwa kwa ajili ya shughul ihii ya usafirishaji wa Mirungi,ukikagua kwa mashaka huwezi gundua kwa mara moja”aliongeza Kamanda Issah.

Alisema hadi sasa watu wawili wanashikiliwa huku akiwataja majina kuwa ni Simoni Boaa mkazi wa Babati  na aliyekuwa dereva wa gari hilo na Abushil Abdalah mkazi wa Kondoa  na kwamba taratibu zikikamilika watafikishwa mahakamani huku akitoa onyo kwa wafanyabiashara wa Mirungi walioshindwa kuacha biashara hiyo .
  






Hivyo makala MBINU MPYA YA KUSAFIRISHA DAWA ZA KULEVYA YABAINIKA

yaani makala yote MBINU MPYA YA KUSAFIRISHA DAWA ZA KULEVYA YABAINIKA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala MBINU MPYA YA KUSAFIRISHA DAWA ZA KULEVYA YABAINIKA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/02/mbinu-mpya-ya-kusafirisha-dawa-za.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "MBINU MPYA YA KUSAFIRISHA DAWA ZA KULEVYA YABAINIKA"

Post a Comment

Loading...