Loading...

IGP SIRRO AMALIZA ZIARA YAKE MKOANI KAGERA NA KUSISITIZA UWELEDI

Loading...
IGP SIRRO AMALIZA ZIARA YAKE MKOANI KAGERA NA KUSISITIZA UWELEDI - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa IGP SIRRO AMALIZA ZIARA YAKE MKOANI KAGERA NA KUSISITIZA UWELEDI, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : IGP SIRRO AMALIZA ZIARA YAKE MKOANI KAGERA NA KUSISITIZA UWELEDI
link : IGP SIRRO AMALIZA ZIARA YAKE MKOANI KAGERA NA KUSISITIZA UWELEDI

soma pia


IGP SIRRO AMALIZA ZIARA YAKE MKOANI KAGERA NA KUSISITIZA UWELEDI

Na Demetrius Njimbwi – Jeshi la Polisi

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro, amewataka askari wa Jeshi hilo kufanyakazi kwa weledi na kwa kuzingatia sheria na taratibu zitakazosaidia kujenga taswira chanya hasa wanapotekeleza majukumu yao ya kila siku.

IGP Sirro, ameyasema hayo alipokutana na kuzungumza na askari na maofisa wa mkoa wa Kagera, wakati akiwa kwenye muendelezo wa ziara zake zenye lengo la kujitambulisha pamoja na kujua changamoto wanazokutananazo wakati wakitekeleza majukumu yao.

Alisema kuwa, kila askari analojukumu mbele yake la kuhakikisha suala la uhalifu na wahalifu linadhibitiwa hususan kwa kuimarisha usalama wa raia na mali zao huku wakizingatia kuwa, mkoa huo unapakana na nchi jirani za Uganda, Rwanda na Burundi.

Hata hivyo, katika ziara yake, IGP Sirro, amewahakikishia askari na maofisa kuwa, yupo tayari kutatua changamoto mbalimbali zinazojitokeza na kuwataka askari kuongeza kasi ya kukabiliana na matishio ya kiuhalifu na wahalifu ili kuifanya jamii kuishi kwa amani na utulivu.

Aidha, katika ziara hiyo, masuala mbalimbali yamejadiliwa huku mbinu mpya za kukabiliana na uhalifu katika mkoa huo pamoja na wilaya zake zikiibuliwa kwa kuzingatia kuimarisha usalama wa raia na mali zao.


Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Simon Sirro (kushoto), akizungumza na Kamanda wa Polisi mkoa wa Kagera, Kamishna Msaidizi Muandamizi wa Polisi (SACP) Augusine Ollomi, muda mfupi alipowasili, IGP Sirro yupo mkoani humo kwa ziara ya kikazi yenye lengo la kujitambulisha na kuzungumza na askari pamoja na kujua chamgamoto wanazokutananazo wakitekeleza majukumu yao. Picha na Demetrius Njimbwi – Jeshi la Polisi.


Hivyo makala IGP SIRRO AMALIZA ZIARA YAKE MKOANI KAGERA NA KUSISITIZA UWELEDI

yaani makala yote IGP SIRRO AMALIZA ZIARA YAKE MKOANI KAGERA NA KUSISITIZA UWELEDI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala IGP SIRRO AMALIZA ZIARA YAKE MKOANI KAGERA NA KUSISITIZA UWELEDI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/07/igp-sirro-amaliza-ziara-yake-mkoani_22.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "IGP SIRRO AMALIZA ZIARA YAKE MKOANI KAGERA NA KUSISITIZA UWELEDI"

Post a Comment

Loading...