Loading...
title : BASATA yazungumzia umuhimu wa masomo ya sanaa mashuleni Kisarawe
link : BASATA yazungumzia umuhimu wa masomo ya sanaa mashuleni Kisarawe
BASATA yazungumzia umuhimu wa masomo ya sanaa mashuleni Kisarawe
Na Agness Francis, Blogu ya Jamii.
Wanafunzi 100 wahitimisha mafunzo ya sanaa ikiwa ni mara ya pili kufanyika katika halimashauri ya wilaya ya kisarawe Mkoani Pwani,ikishirikisha shule 5 kutoka katika wilaya hiyo ambazo ni Chanzige A,ChanzigeB,Kibasila,Kazimzumbwi pamoja na Sanze .
Nae muwakilishi wa mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Simon Biginagwa amezungumza hayo leo katika Halimashauri ya wilaya ya Kisarawe Mkoa wa Pwani amesema kuwa sasa ni wakati wa kuendeleza utamaduni wetu wa kitanzania badala ya tamaduni na mila za kizungu akiongezea kuwa kupia tamaduni zetu hupata fursa ya kuweza kupa ajira na amesisitiza pia kulinda amani nchini .
Hata hivyo Mkurugenzi Ukuzaji Sanaa na Masoko Basata Vivian Shalua amemshukuru mkuu wa wilaya ya kisarawe kwa kuwapa kibali cha kuweza kufanya mafunzo ya sanaa kwa wanafunzi hao na ;NIvizuri watoto kufanya sanaa wakiwa mashuleni na Lengo ikiwa ni kukuza viapaji vya watoto na kufufua ngoma zetu za utamaduni; amesema Mkurugenzi huyo.
Afisa elimu Halimashauri ya kisarawe Zipporah Daniel Simwanza, amewapongeza basata kwa kuweza kurudi tena katika Halmashauri hiyo kuweza kufanya zoezi hilo la uandaaji wa kutoa mafunzo ya sanaa kwa wanafunzi hao .
Vilevile Afisa maendeleo ya jamii Halimashauri ya Kisarawe Wanchoke Juma ametoa wito kwa walimu kufundisha watoto mafuzo ya sanaa mashuleni na kulichukulia somo la sanaa kama masomo mengine badala ya kulifanya kama la ziada.
Mkurugenzi Ukuzaji Sanaa na Masoko Basata Vivian Shalua, akizungumza na wanafunzi wa shule za Kisarawe juu ya umuhimu wa kuendeleza sanaa na tamaduni za kitanzania leo katika Halimauri ya Kisarawe Mkoani pwani.
Afisa Elimu Halimashauri ya Kisarawe, Zipporah Daniel Simwanza akizungumza na wanafunzi wa Halimashauri ya Kisarawe na kuwapongeza kwa kujitokeza kwa wingi katika kupata mafunzo ya sanaa yalioandaliwa na Basata na kuwataaka wanafuzi hao kudumisha tamaduni zetu leo katika Halimashauri ya mji wa Kisarawe Mkoa wa Pwani.
Mwakilishi wa mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Simon Biginagwa, akizungumza na wanafunzi hao akiwataka pia kuendeleza utamaduni wetu badala ya kuiga ule wa kizungu kwani sanaa ni chanzo cha ajira na kutoa wito kwa wazazi kuwaruhu watoto kushiriki mafunzo hayo ya sanaa leo katika hafla ya kuhitimisha mafunzo hayo Halmashauri ya Kisarawe Mkoani Pwani
Baadhi ya wanafunzi wa Shule za msingi za Kisarawe wakitoa burudani ya kuimba na kucheza ya ngoma za asaili mojawapo kati ya mafunzo waliyopata kwa viongozi, waandishi wa habari pamoja na walimu wao leo katika hafla ya kuhitimisha mafunzo hayo Halmashauri ya Kisarawe Mkoani Pwani .
Picha ya pamoja wakiwepo viongozi wa Kisarawe waandaaji wa mafuzo hayo Basata pamoja na walimu waliofundisha saana hizo mbalimbali ikiwemo kuimba, kucheza nyimbo za tamaduni ya asili ya Mtanzania leo katika hafla ya kuhitimisha mafunzo hayo Halmashauri ya Kisarawe Mkoani Pwani. (Picha na Agness Francis, Blogu ya Jamii)
Hivyo makala BASATA yazungumzia umuhimu wa masomo ya sanaa mashuleni Kisarawe
yaani makala yote BASATA yazungumzia umuhimu wa masomo ya sanaa mashuleni Kisarawe Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala BASATA yazungumzia umuhimu wa masomo ya sanaa mashuleni Kisarawe mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/09/basata-yazungumzia-umuhimu-wa-masomo-ya.html
0 Response to "BASATA yazungumzia umuhimu wa masomo ya sanaa mashuleni Kisarawe"
Post a Comment