Loading...

DKT. ASHATU KIJAJI AZINDUA KITABU CHA MWONGOZO KWA WANAMIPANGO

Loading...
DKT. ASHATU KIJAJI AZINDUA KITABU CHA MWONGOZO KWA WANAMIPANGO - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa DKT. ASHATU KIJAJI AZINDUA KITABU CHA MWONGOZO KWA WANAMIPANGO, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : DKT. ASHATU KIJAJI AZINDUA KITABU CHA MWONGOZO KWA WANAMIPANGO
link : DKT. ASHATU KIJAJI AZINDUA KITABU CHA MWONGOZO KWA WANAMIPANGO

soma pia


DKT. ASHATU KIJAJI AZINDUA KITABU CHA MWONGOZO KWA WANAMIPANGO


Benny Mwaipaja, Dodoma.

Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji, amezindua Kitabu cha Mwongozo kwa Wanamipango Tanzania, kilichoandaliwa na Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini kwa kushirikiana na Taasisi ya Mafunzo ya Jamii ya nchini Uholanzi (ISS), na kuwataka wataalamu wa mipango hapa nchini kuandaa mipango yenye tija itakayoiwezesha jamii kuondokana na umasikini.

Dkt. Kijaji ameeleza kuwa nafasi ya wataalamu wa mipango katika kukuza uchumi wa nchi ni kubwa na kwamba kinachotakiwa ni kuandaa mipango shirikishi itakayochangia kuimarisha maisha ya wananchi ili waweze kujikwamua kiuchumi.

“Ni matumaini yangu makubwa kwamba kuzinduliwa kwa kitabu hiki cha mwongozo kwa wanamipango, kutakuwa chachu ya wataalamu wetu kuangalia namna ya kupeleka maendeleo vijijini na sehemu nyingine duniani kwa kutoa wataalamu waliobobea ili kuharakisha maendeleo ya nchi” alisistiza Dkt. Kijaji

Ameeleza kuwa maudhui ya kitabu hicho yapelekwe hadi ngazi za chini kupitia Serikali za Mitaa ili watu wengi waweze kukisoma na kuelekezwa namna bora ya kupanga mipango yao ya maendeleo.

Kwa upande wake Kaimu Mkuu wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijini, Prof. Hozen Mayaya, amesema kitabu hicho kimelenga kuwaongezea ujuzi wataalamu wa mipango kwa kuzingatia vitendo zaidi badala ya nadharia.

“Kitabu cha Mwongozo kwa wanamipango kitakuwa rejea ya nadharia nyingi na njia ambazo wataalamu wanapaswa kuzijua, namna ya kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi na kuifanya mipango iweze kutekelezeka kama ilivyokusudiwa” alisema Prof. Mayaya.
 Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) (aliyeshika mkasi) akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa kitabu cha Mwongozo kwa Wanamipango (Planners handbook), Toleo la Pili, kilichoandikwa na Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini kwa kushirikiana na Taasisi ya Mafunzo ya Jamii ya nchini Uholanzi (ISS), tukio hilo limefanyika katika Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini, Kampasi ya Dodoma.
 Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), (katikati), akionesha kitabu cha Mwongozo kwa Wanamipango (Planners Handbook), Toleo la Pili,  baada ya kukizindua rasmi katika Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini-Dodoma. Wa pili kushoto ni Kaimu Balozi wa Uholanzi hapa nchini, Bi. Lianne Houben, na wa pili kulia ni Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi la Chuo hicho Prof. Razack Lokina.
 Kaimu Balozi wa Uholanzi hapa Nchini, Bi. Lianne Hauben (kushoto), akifurahi wakati akikabidhiwa na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), nakala ya Kitabu cha Mwongozo kwa Wanamipango (Planners Handbook), Toleo la Pili, mara baada ya kukizindua rasmi mkoani Dodoma.
 Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), akiwaongoza wadau mbalimbali kunyanyua nakala ya kitabu cha Mwongozo kwa Wanamipango (Planners handbook), Toleo la Pili, kilichoandikwa na Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini kwa kushirikiana na Taasisi ya Mafunzo ya Jamii ya nchini Uholanzi (ISS), tukio hilo limefanyika katika Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini, Kampasi ya Dodoma.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA


Hivyo makala DKT. ASHATU KIJAJI AZINDUA KITABU CHA MWONGOZO KWA WANAMIPANGO

yaani makala yote DKT. ASHATU KIJAJI AZINDUA KITABU CHA MWONGOZO KWA WANAMIPANGO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala DKT. ASHATU KIJAJI AZINDUA KITABU CHA MWONGOZO KWA WANAMIPANGO mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/09/dkt-ashatu-kijaji-azindua-kitabu-cha.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "DKT. ASHATU KIJAJI AZINDUA KITABU CHA MWONGOZO KWA WANAMIPANGO"

Post a Comment

Loading...