Loading...
title : FEDHA ZA UPANUZI VITUO VYA AFYA ZIFANYE KAZI ILIYOTARAJIWA- RC GALLAWA
link : FEDHA ZA UPANUZI VITUO VYA AFYA ZIFANYE KAZI ILIYOTARAJIWA- RC GALLAWA
FEDHA ZA UPANUZI VITUO VYA AFYA ZIFANYE KAZI ILIYOTARAJIWA- RC GALLAWA
Grace Gwamagobe-Songwe.
Mkuu wa Mkoa wa Songwe Chiku Gallawa amesema atahakikisha anasimamia kwa ukaribu fedha zilizotolewa na serikali Mkoani hapa kwa ajili ya upanuzi wa vituo vya afya ili zifanye kazi zaidi ya ile iliyopangwa awali kutokana na kuongezeka kwa nguvu za wananchi.
Gallawa ameyasema hayo mapema jana wakati wa ziara yake Wilaya ya Mbozi alipokagua maendeleo ya upanuzi wa vituo vya afya vya Isansa kilichopokea milioni 500 na kituo cha Afya cha Iyula Kilichopokea milioni 400, kwa ajili ya ujenzi wa maabara, nyumba ya daktari, chumba cha upasuaji, jengo la mama na mtoto na chumba cha kuhifadhia maiti.
“Fedha hizi lazima zifanye kazi iliyopangwa vizuri na pia tuongeze kazi nyingine ya ziada kutokana na kuwa tumepata nguvu ya wananchi lakini pia mafundi wetu hawa tunaowatumia ni wazawa na wenyeji wa maeneo ya kwetu kwahiyo gharama zao zitatupa unafuu ambao tunatakiwa kuutumia kuongeza kazi nyingine”, amesema Gallawa.
Ameongeza kuwa licha ya upanuzi wa vituo vya afya kuchelewa kuanza bado ana Imani kuwa wataweza kumaliza ndani ya muda uliopangwa kutokana na uchapakazi wa mafundi wazawa wa maeneo hayo.
Mkuu wa Mkoa wa Songwe Chiku Gallawa akizungumza na mafundi wanaojenga katika kituo cha Afya Isansa Wilaya ya Mbozi, kituo hicho cha Afya kimepokea shilingi milioni 500 kwa ajili ya upanuzi wa kituo hicho.
Mkuu wa Mkoa wa Songwe Chiku Gallawa akizungumza na baadhi ya watendaji na wananchi wa kijiji cha Iyula waliojitokeza katika eneo la ujenzi katika kituo cha Afya cha Iyula Wilaya ya Mbozi, kituo hicho cha Afya kimepokea shilingi milioni 400 kwa ajili ya upanuzi wa kituo hicho.
Hivyo makala FEDHA ZA UPANUZI VITUO VYA AFYA ZIFANYE KAZI ILIYOTARAJIWA- RC GALLAWA
yaani makala yote FEDHA ZA UPANUZI VITUO VYA AFYA ZIFANYE KAZI ILIYOTARAJIWA- RC GALLAWA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala FEDHA ZA UPANUZI VITUO VYA AFYA ZIFANYE KAZI ILIYOTARAJIWA- RC GALLAWA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/04/fedha-za-upanuzi-vituo-vya-afya-zifanye.html
0 Response to "FEDHA ZA UPANUZI VITUO VYA AFYA ZIFANYE KAZI ILIYOTARAJIWA- RC GALLAWA"
Post a Comment