Loading...

Puma Energy kuchangamkia fursa ukuaji wa sekta ya anga.

Loading...
Puma Energy kuchangamkia fursa ukuaji wa sekta ya anga. - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Puma Energy kuchangamkia fursa ukuaji wa sekta ya anga., tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Puma Energy kuchangamkia fursa ukuaji wa sekta ya anga.
link : Puma Energy kuchangamkia fursa ukuaji wa sekta ya anga.

soma pia


Puma Energy kuchangamkia fursa ukuaji wa sekta ya anga.

KAMPUNI ya mafuta ya Puma Energy Tanzania imepanga kutumia vyema mageuzi yanayoendelea katika sekta ya anga nchini kwa kuboresha zaidi huduma zake ili ziandane na kasi ya ukuaji wa sekta hiyo.

Kwa mujibu wa Meneja Idara ya Mafuta ya Ndege wa kampuni hiyo, Raymond Tungaraza, kwasasa kampuni hiyo inaandaa mikakati itayoiwezesha kujitanua ili kunufaika zaidi na ongezeko la idadi ya ndege za kitaifa na kimataifa linalotarajiwa kufuatia mageuzi hayo.

“Tunachokifanya Puma Energy ni kuhakikisha tunakwenda sambamba na mabadiliko yanayoendelea katika sekta ya anga’’ alisema Tungaraza katika mahojiano yake na waandishi wa habari hivi karibuni katika Mkutano wa wadau wa sekta ya anga barani Afrika ulioandaliwa na Umoja Wa Mashirika ya Ndege barani Afrika (AFRAA) kwa kushirikiana na Kampuni ya Ndege nchini (ATCl) uliofanyika visiwani Zanzibar hivi karibuni.

Alitolea mfano wa maboresho yaliyofanywa na kampuni hiyo katika mfumo wake wa huduma ya mafuta ya ndege katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) ili kuwezesha kampuni hiyo kukidhi mahitaji ya usambazaji wa nishati hiyo ambayo yanayotarajiwa kuongezeka mara tu baada ya kukamilika kwa upanuzi unaoendelea wa jengo la tatu la abiria (Terminal three).

Alisema lengo la kampuni hiyo katika sekta ya anga ni kutoa huduma ya mafuta kwa bei ya ushindani kwa wateja wake huku pia ikizingatia kutoa huduma hizo kwa kukidhi mahitaji ya viwango usalama na ubora wa kimataifa.

"Linapokuja suala la usambazi wa mafuta ya ndege huwa tunajitahidi sana kuhakikisha tunawapa urahisi zaidi wateja wetu kwa kuhakikisha tunaratibu kila kitu sisi kuanzia uagizaji, utunzaji, uhifadhi na usafiri hadi kwenye vituo vyetu vilivyopo kwenye viwanja vya ndege kwa kutumia rasilimali watu wenye weledi zaidi katika suala hilo,’’ .

“Ni wazi tumejenga sifa nzuri katika utoaji wa huduma zetu kutokana na ufanisi wetu, rekodi nzuri katika masuala ya usalama pamoja na bei yenye ushindani,’’ alitaja.


Hivyo makala Puma Energy kuchangamkia fursa ukuaji wa sekta ya anga.

yaani makala yote Puma Energy kuchangamkia fursa ukuaji wa sekta ya anga. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Puma Energy kuchangamkia fursa ukuaji wa sekta ya anga. mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/04/puma-energy-kuchangamkia-fursa-ukuaji.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "Puma Energy kuchangamkia fursa ukuaji wa sekta ya anga."

Post a Comment

Loading...