Loading...

BENKI YA EXIM TANZANIA YAKAMILISHA KAMPENI YA UCHANGISHAJI DAMU NCHI NZIMA.

Loading...
BENKI YA EXIM TANZANIA YAKAMILISHA KAMPENI YA UCHANGISHAJI DAMU NCHI NZIMA. - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa BENKI YA EXIM TANZANIA YAKAMILISHA KAMPENI YA UCHANGISHAJI DAMU NCHI NZIMA., tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : BENKI YA EXIM TANZANIA YAKAMILISHA KAMPENI YA UCHANGISHAJI DAMU NCHI NZIMA.
link : BENKI YA EXIM TANZANIA YAKAMILISHA KAMPENI YA UCHANGISHAJI DAMU NCHI NZIMA.

soma pia


BENKI YA EXIM TANZANIA YAKAMILISHA KAMPENI YA UCHANGISHAJI DAMU NCHI NZIMA.

Afisa uhamasishaji wa mpango wa taifa wa Damu salama, Mariam Juma akimpima damu mfanyakazi wa Exim Bank Daniel Lukuba wakati wa kampeni ya uhamasishaji watu kuchangia damu kwa hiari kwa kushirikiana na Damu Salama iliyofanyika kwenye makao makuu ya benki hiyo, posta mjini Dar es Salaam kuadhimisha siku ya watoaji damu duniania (World Blood Donors Day 2018). 
Afisa Muuguzi kutoka Mpango wa Taifa wa Damu Salama akimtoa damu mfanyakazi wa Exim Bank Patrick Masawe wakati wa kampeni ya uhamasishaji watu kuchangia damu kwa hiari kwa kushirikiana na Damu Salama iliyofanyika kwenye makao makuu ya benki hiyo, posta mjini Dar es Salaam kuadhimisha siku ya watoaji damu duniani (World Blood Donors Day 2018). 
Baadhi ya wafanyakazi wa benki ya Exim waitoa damu.

KUFIKIA 14 Juni, 2018 benki ya Exim Tanzania ilifikia kilele cha kampeni inayoenda kwa jina la "Kupata damu katika benki ya damu kesho, leo" ambayo imejikita kuwahamasisha wananchi kuchangia damu ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya uchangiaji damu inayofanyika kila tarehe 14 Juni duniani kote.

Lengo kuu la kampeni hiyo ambayo iliendana sambamba na kauli mbiu ya benki hiyo inayosema “Exim kazini leo kwa ajili ya kesho” ni kuchangisha damu na kutoa elimu ya umuhimu wa kuchangia damu katika mpango wa taifa. Kampeni hiyo inaonyesha kuwa benki ya Exim iko makini kutafuta njia za ubunifu za kuhudumia wateja wake na muhimu zaidi, inajitolea kuhakikisha inashirki kuleta mabadiliko chanya katika jamii.

Mpango huu kila mwaka unalenga kukusanya damu kwa ajili ya benki ya taifa chini ya usimamizi wa Mpango wa Taifa wa uchangiaji damu nchini [NBTS].

Kampeni hii ilianza rasmi katika tawi la Exim mkoani Arusha tarehe 4 Juni na kuendelea katika mikoa ya Mbeya, Dodoma na Mwanza. Tukio kuu limefanyika katika makao makuu ya benki hiyo jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na wafanyakazi 200 , wateja na jamii chini ya kauli mbiu ya kimataifa: " “Jitoe kwa ajili ya mwingine. Changia damu." Kampeni hii inakumbusha jukumu la kila mtu kujitolea katika kuwasaidia wengine katika hali ya dharura kwa kutoa zawadi ya thamani ya damu. Pia inasisitiza juu ya ukweli kwamba ni muhimu kutoa damu mara kwa mara ili kuhakikisha kuwepo na damu ya kutosha kabla ya dharura kujitokeza. Kampeni hii ni sehemu ya programu ya majukumu ya shirika la kijamii ya benki ya Exim Tanzania iitwayo, Exim Cares. 


Hivyo makala BENKI YA EXIM TANZANIA YAKAMILISHA KAMPENI YA UCHANGISHAJI DAMU NCHI NZIMA.

yaani makala yote BENKI YA EXIM TANZANIA YAKAMILISHA KAMPENI YA UCHANGISHAJI DAMU NCHI NZIMA. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala BENKI YA EXIM TANZANIA YAKAMILISHA KAMPENI YA UCHANGISHAJI DAMU NCHI NZIMA. mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/06/benki-ya-exim-tanzania-yakamilisha.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "BENKI YA EXIM TANZANIA YAKAMILISHA KAMPENI YA UCHANGISHAJI DAMU NCHI NZIMA."

Post a Comment

Loading...