Loading...

Bandari ya Mtwara kupokea mafuta tani 8000 mwezi Septemba

Loading...
Bandari ya Mtwara kupokea mafuta tani 8000 mwezi Septemba - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Bandari ya Mtwara kupokea mafuta tani 8000 mwezi Septemba, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Bandari ya Mtwara kupokea mafuta tani 8000 mwezi Septemba
link : Bandari ya Mtwara kupokea mafuta tani 8000 mwezi Septemba

soma pia


Bandari ya Mtwara kupokea mafuta tani 8000 mwezi Septemba

Na Nuru Mwasampeta, Dodoma
Imeelezwa kuwa Bandari ya Mtwara itapokea mafuta tani za ujazo 8000 (lita milioni 9.6) ifikapo mwezi Septemba mwaka huu ikiwa ni mara ya Pili kupokea shehena hiyo ya mafuta kutoka yaliposhushwa kwa mara ya kwanza mwezi Juni mwaka huu.

Hayo yamebainishwa leo tarehe 29 Agosti, 2018 na Kaimu Mkurugenzi wa Wakala wa Uagizaji Mafuta kwa Pamoja (PBPA), Mjiolojia Erasto Simon, alipokuwa akiwasilisha ripoti ya Wizara ya Nishati kuhusu uanzishwaji wa gati la kupokelea mafuta katika bandari ya Mtwara kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini  jijini Dodoma.

Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu na Katibu Mkuu wa Wizara, Dkt. Hamisi Mwinyimvua waliwaongoza Watendaji mbalimbali wa Wizara na Taasisi zake katika utoaji wa taarifa na ufafanuzi wa masuala mbalimbali yaliyojitokeza.

“ Kiasi cha tani za ujazo 8,000 kinatarajiwa kushushwa katika Bandari ya Mtwara ifikapo mwezi Septemba ambapo tani 5,000 kati ya hizo zitakuwa ni mafuta ya dizeli na tani 3,000 zitakuwa ni petroli,” alisema Simon.

Ameongeza kuwa, Serikali iliamua kutumia rasmi Bandari ya Mtwara kupokea mafuta ili kupunguza msongamano wa magari ya kusafirisha mafuta kwenda mikoa ya Kusini na nchi jirani.

Amebainisha kuwa, kwa mara ya kwanza mafuta yalipokelewa katika bandari ya Mtwara tarehe 28 Juni, 2018 ambapo kiasi cha tani 8,339 kilishushwa bandarini hapo na kupokelewa kwenye maghala ya kuhifadhi mafuta yanayomilikiwa na kampuni za GM & Company /Oryx na Oilcom Tanzania.
 Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini pamoja na ujumbe kutoka Wizara ya Nishati na Taasisi zake ukiongozwa na Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu na Katibu Mkuu wa Wizara, Dkt. Hamisi Mwinyimvua wakiwa katika kikao kilichojadili taarifa mbili za utekelezaji wa majukumu ya  Wakala wa Uagizaji Mafuta kwa Pamoja (PBPA) na Shirika la Taifa la Maendeleo ya Petroli (TPDC) jijini Dodoma.
 Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (wa kwanza kushoto) na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Dkt Hamisi Mwinyimvua (wa Pili kushoto) wakiongoza Ujumbe wa Wizara pamoja na Taaisisi zake katika kikao na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini.


KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA



Hivyo makala Bandari ya Mtwara kupokea mafuta tani 8000 mwezi Septemba

yaani makala yote Bandari ya Mtwara kupokea mafuta tani 8000 mwezi Septemba Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Bandari ya Mtwara kupokea mafuta tani 8000 mwezi Septemba mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/08/bandari-ya-mtwara-kupokea-mafuta-tani.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "Bandari ya Mtwara kupokea mafuta tani 8000 mwezi Septemba"

Post a Comment

Loading...