Loading...
title : MOROGORO MARATHON 2018 KUFANYIKA DESEMBA 2 ,ZOEZI LA UANDIKISHAJI WASHIRIKI LAANZA.
link : MOROGORO MARATHON 2018 KUFANYIKA DESEMBA 2 ,ZOEZI LA UANDIKISHAJI WASHIRIKI LAANZA.
MOROGORO MARATHON 2018 KUFANYIKA DESEMBA 2 ,ZOEZI LA UANDIKISHAJI WASHIRIKI LAANZA.
ZAIDI ya washiriki 5000 kutoka mikoa ya Morogoro,Dodoma,Dar es Salaam ,Iringa na Zanzibar wanataraji kushiriki mbio mpya za Marathoni zijulikanazo kama “Morogoro Marathon 2018” zitakazofanyika katika mji wa Morogoro kwa mara ya kwanza Desemba 2 mwaka huu.
Miongoni mwa washiriki hao wamo pia wanariadha wanaoshiriki mashindano ya Kimataifa wa Tanzania na nchi jirani za Kenya ,Ethiopia na Sudani ya Kusini watakaochuana kuweka rekodi mpya katika riadha kutokana na hali ya hewa ya mji wa Morogoro.
Meneja Uhusiano na Masoko wa taasisi ya uwakala wa Michezo ya Itete “ITETE SPORTS AGENCY” ambao ndio waandaaji wa Mbio hizo ,Dixon Busagaga alisema tukio hilo litakuwa tukio la kwanza kubwa kuwahi kufanyika katika mkoa wa Morogoro na kukutanisha idadi kubwa ya washiriki.
“Kutokana na jiografia ya mkoa wa Morogoro kuwa lango la mikoa ya mikoa ya kusini na kupakana kwa ukaribu na baadhi ya mikoa ya nyanda za kati na Pwani ni wazi matazamio yetu litakuwa tukio kubwa kwa mkoa wa Morogoro”alisema Busagaga.“Tukio hili limebeba maudhui matatu makubwa ambayo ni ,uhamasishaji wa masula ya utunzaji wa Mazingira ,uhamasishaji katika masuala ya Afya pamoja na kutangaza vivutio vya utalii hasa vilivyopo kusini mwa nchi yetu . “alisema Busagaga .
Busagaga alisema hadi sasa vilabu zaidi ya 50 vya mazoezi “Jogging Clubs” kutoka mikoa ya Dar es Salaam ,Dodoma na Morogoro vimewasilisha maombi ya kushiriki katika tukio hilo pamoja na Vilabu zaidi ya 20 vya timu za mpira wa miguu za wachezaji wa zamani yaani Veterani.
“Tukio hili tunataka kulifanya la pekee,tutakuwa na siku mbili za tukio,siku moja kabla ya tukio kubwa la mbio,tutakuwa na shughuli za kuotesha miti zaidi ya 10,000 katika maeneo mbalimbali ya mji wa Morogoro”alisema Busagaga.
“Baada ya tukio hilo ,Timu za Veterani zitakazokuwa zimewasili na kujisalijili kwa ajili ya ushiriki wa Marathoni hiyo tumeandaa mashindano yao kwa jioni ya Desemba mosi ,ambapo washindi wa Bonanza hilo watakabidhiwa zawadi zao na mgeni rasmi siku ya tukio la Marathon.”alisema Busagaga
Hivyo makala MOROGORO MARATHON 2018 KUFANYIKA DESEMBA 2 ,ZOEZI LA UANDIKISHAJI WASHIRIKI LAANZA.
yaani makala yote MOROGORO MARATHON 2018 KUFANYIKA DESEMBA 2 ,ZOEZI LA UANDIKISHAJI WASHIRIKI LAANZA. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MOROGORO MARATHON 2018 KUFANYIKA DESEMBA 2 ,ZOEZI LA UANDIKISHAJI WASHIRIKI LAANZA. mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/11/morogoro-marathon-2018-kufanyika.html
0 Response to "MOROGORO MARATHON 2018 KUFANYIKA DESEMBA 2 ,ZOEZI LA UANDIKISHAJI WASHIRIKI LAANZA."
Post a Comment