Loading...
title : DC KARATU ATOA ONYO KWA WATAKAOKWAMISHA UPIMAJI ARDHI YA VIJIJI
link : DC KARATU ATOA ONYO KWA WATAKAOKWAMISHA UPIMAJI ARDHI YA VIJIJI
DC KARATU ATOA ONYO KWA WATAKAOKWAMISHA UPIMAJI ARDHI YA VIJIJI
Mkuu wa wilaya ya Karatu,Theresia Mahongo amewaonya wananchi wanaowashawishi wenzao kukataa ardhi ya vijiji vyao isipimwe na kupangiwa matumizi bora ya ardhi kuwa serikali haitasita kuwachukulia hatua kali za kisheria .
Akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi Hati ya Kimila ya maeneo ya malisho kwa uongozi wa Kijiji cha Endesh Kata ya Baray jana amesema utaratibu wa kupima na kupanga matumizi bora ya ardhi una baraka za serikali na unalenga kupunguza migogoro ya ardhi kati ya wafugaji,wakulima na wawekezaji.
‘Serikali haitawaonea huruma wanaokwamisha juhudi za serikali kuhakikisha tunakua na vijiji vyenye ramani zinazotambulika kisheria na ambazo wananchi wamekubaliana namna ya matumizi ya ardhi katika shughuli za maendeleo,”amesema Mahongo
Amewataka wananchi kutoa ushirikiano kwa wataalam wa ardhi wanaofika katika maeneo yao kwaajili ya kupima na kupanga matumizi bora ya ardhi kwamba ni jambo zuri ambalo lina faida kubwa katika kujipangia mipango ya maendeleo.
Wafugaji wa jamii ya Wabarbaig katika Kijiji cha Endesh Kata ya Baray wilaya ya Karatu mkoa wa Arusha wakiimba nyimbo za asili wakati wa hafla ya kukabidhiwa hati ya kimila yenye mpango wa matumizi bora ya ardhi na nyanda za malisho iliyoandaliwa na Ujamaa Community Resouce Team(UCRT).
Mkuu wa wilaya ya Karatu mkoa wa Arusha,Theresia Mahongo(kulia) akiwa ameungana na Wanawake wa jamii ya kifugaji ya Wabarbaig katika Kijiji cha Endesh Kata ya Baray wakiimba nyimbo za asili.
Mkuu wa wilaya ya Karatu mkoa wa Arusha,Theresia Mahongo(kulia) akimkabidhi Hati ya Kimila Mwenyekiti wa Kijiji cha Endesh Kata ya Baray ,Geway Nanagi kutoka jamii ya kifugaji ya Wabarbaig wakati wa hafla ya kukabidhiwa hati ya mpango wa matumizi bora ya ardhi na nyanda za malisho iliyoandaliwa na Ujamaa Community Resouce Team(UCRT).
Mzee wa jamii ya kifugaji ya Wabarbaig katika Kijiji cha Endesh Kata ya Baray wilaya ya Karatu,mkoa wa Arusha,Gidaulanda Marakwa akifurahia Hati ya Kimila iliyoandaliwa na taasisi ya Ujamaa Community Resources Team.Picha na Filbert Rweyemamu.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala DC KARATU ATOA ONYO KWA WATAKAOKWAMISHA UPIMAJI ARDHI YA VIJIJI
yaani makala yote DC KARATU ATOA ONYO KWA WATAKAOKWAMISHA UPIMAJI ARDHI YA VIJIJI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala DC KARATU ATOA ONYO KWA WATAKAOKWAMISHA UPIMAJI ARDHI YA VIJIJI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/12/dc-karatu-atoa-onyo-kwa-watakaokwamisha.html
0 Response to "DC KARATU ATOA ONYO KWA WATAKAOKWAMISHA UPIMAJI ARDHI YA VIJIJI"
Post a Comment