Loading...

Rukwa wapokea vifaa vya Shilingi Milioni 211 kuboresha huduma za afya ya uzazi na mtoto

Loading...
Rukwa wapokea vifaa vya Shilingi Milioni 211 kuboresha huduma za afya ya uzazi na mtoto - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Rukwa wapokea vifaa vya Shilingi Milioni 211 kuboresha huduma za afya ya uzazi na mtoto, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Rukwa wapokea vifaa vya Shilingi Milioni 211 kuboresha huduma za afya ya uzazi na mtoto
link : Rukwa wapokea vifaa vya Shilingi Milioni 211 kuboresha huduma za afya ya uzazi na mtoto

soma pia


Rukwa wapokea vifaa vya Shilingi Milioni 211 kuboresha huduma za afya ya uzazi na mtoto



Mradi wa uzazi salama Mkoani Rukwa umekabidhi vifaa tiba vyenye thamani ya Shilingi 211,145,850/= kwa ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Rukwa ili kuvisambaza katika vituo 198 vya kutolea huduma za afya, ikiwa ni muendelezo wa jitihada na dhamira yao ya kuhakikisha wanashirikiana na Mkoa katika kuboresha huduma za afya ya uzazi na mtoto katika Mkoa.

Mradi huo unaoundwa kwa ushirikiano wa mashirika matatu ya Plan International Tanzania, AFRICARE na JHPIEGO kwa ufadhili wa serikali ya watu wa Canada umekabidhi vifaa hivyo vikiwemo vitanda vya kujifungulia, vifaa vya upasuaji kwa kinamama wajawazito, vifaa vya kumsaidia mtoto mchanga na mama kupumua, vifaa vya kuwasaidia watoto njiti, majokofu ya kuhifadhia damu na vifaa vya kufanyia tathmini ya hali ya lishe kwa watoto wenye umri chini ya miaka mitano.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo aliwaagiza wakurugenzi wa halmashauri kuhakikisha wanaratibu kufanyika kwa siku ya afya kwa mwaka mara moja kwa kila kijiji na kuwataka wakuu wa wilaya wasimamie zoezi hilo. Na kuwaomba wanaume, wazee na viongozi wote wa dini pamoja na vijiji kutambua jukumu la afya ya uzazi na mtoto pamoja na familia ni la wote na sio la kinamama na wanawake peke yao.

“Viongozi wa serikali katika ngazi za vijiji na kata wanao wajibu wa kuhakikisha akina mama wanahudhuria katika vituo vya afya pindi wanapojigundua ni wajawazito kwa huduma na ushauri wa kiafya. Tuwe mstari wa mbele kuelimisha wengine hasa vijana wetu kuhusu afya ya uzazi na kuwasisitiza kushiriki katika matukio mbalimbali yahusuyo afya kama huduma rafiki kwa vijana na siku ya afya ya kijiji “village health day” yanayoratibiwa na mradi wa Uzazi Salama.”

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo ( wa pili toka kulia) akipewa maelezo ya kitaalamu juu ya matumizi ya vifaa tiba vilivyotolewa na mradi wa Uzazi Salama na mmoja wa wawakilishi wa mradi huo (wa kwanza Kulia). 
Baadhi ya Vifaa tiba vilivyotolewa na mradi wa Uzazi salama Mkoa wa Rukwa kwa Ofsi ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa. 
Mkuu wa mkoa wa Rukwa Mh.Joachim Wangabo. Wakuu wa Wilaya za Sumbawanga, Kalambo na NKasi (kushoto) wakiweka saini mkataba wa usimamizi wa huduma za afya ya uzazi na mtoto mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo (kulia) katika hafla fupi ya  uzinduzi wa Kampeni ya “JIONGEZE TUWAVUSHE SALAMA” katika Mkoa wa Rukwa.



Hivyo makala Rukwa wapokea vifaa vya Shilingi Milioni 211 kuboresha huduma za afya ya uzazi na mtoto

yaani makala yote Rukwa wapokea vifaa vya Shilingi Milioni 211 kuboresha huduma za afya ya uzazi na mtoto Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Rukwa wapokea vifaa vya Shilingi Milioni 211 kuboresha huduma za afya ya uzazi na mtoto mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/12/rukwa-wapokea-vifaa-vya-shilingi.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "Rukwa wapokea vifaa vya Shilingi Milioni 211 kuboresha huduma za afya ya uzazi na mtoto"

Post a Comment

Loading...