Loading...

Wakuu wa Mikoa, Makatibu Tawala wa Mikoa Tanzania Bara Kushiriki katika Mafunzo ya Uongozi

Loading...
Wakuu wa Mikoa, Makatibu Tawala wa Mikoa Tanzania Bara Kushiriki katika Mafunzo ya Uongozi - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Wakuu wa Mikoa, Makatibu Tawala wa Mikoa Tanzania Bara Kushiriki katika Mafunzo ya Uongozi, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Wakuu wa Mikoa, Makatibu Tawala wa Mikoa Tanzania Bara Kushiriki katika Mafunzo ya Uongozi
link : Wakuu wa Mikoa, Makatibu Tawala wa Mikoa Tanzania Bara Kushiriki katika Mafunzo ya Uongozi

soma pia


Wakuu wa Mikoa, Makatibu Tawala wa Mikoa Tanzania Bara Kushiriki katika Mafunzo ya Uongozi

Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala wa Mikoa hamsini na mbili wa Tanzania Bara wanatarajiwa kushiriki katika programu ya mafunzo ya uongozi kwa kipindi cha wiki moja kuanzia Jumatatu ya tarehe 3 Disemba, 2018 hadi Ijumaa ya tarehe 7 Disemba, 2018, mkoani Dodoma. 

Warsha hiyo ya mafunzo ambayo imeandaliwa na Taasisi ya UONGOZI kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) itafunguliwa rasmi na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb) leo. 

Kwa mujibu wa Taasisi ya UONGOZI, programu hii ya mafunzo ya uongozi, ni ya kwanza ya aina yake iliyoandaliwa mahususi kwa ajili ya Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala wa Mikoa. 

“Lengo la programu hii ni kuimarisha uwezo wa Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala katika kufanya maamuzi ya kimkakati, kuongoza watu na kusimamia rasilimali nyingine, pamoja na kujijengea sifa binafsi za uongozi,” alisema Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi hiyo, Prof. Joseph Semboja. 

Prof. Semboja pia alisema, “Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala wa Mikoa wana nafasi muhimu katika kuwezesha ukuaji na maendeleo ya nchi. Hivyo, tunatarajia kwamba kupitia programu hii, uwezo wao wa kuongoza utaimarika na kuwawezesha kuchangia katika jitihada za kuleta maendeleo endelevu nchini na hatimaye, barani mwetu.” 

Prof. Semboja aliongezea kwamba huu ni mwendelezo wa jitihada za Taasisi ya UONGOZI na Ofisi ya Rais, TAMISEMI zinazolenga kuwafikia viongozi wengi iwezekanavyo wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa ili kupanua uelewa wa masuala ya uongozi na kuongeza tija ya shughuli wanazozifanya za kuwatumikia wananchi. Kati ya Mei 2017 na Oktoba 2018, mafunzo ya uongozi yalitolewa kwa Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri za Majiji, Manispaa na Wilaya, kwa awamu tano tofauti. 

Warsha hiyo ya mafunzo ya siku tano itajumuisha mada kuu zifuatazo; Uongozi Binafsi na Akili Hisia, Mwingiliano na Mahusiano baina ya Viongozi wa Kisiasa na Viongozi Watendaji, Mawasiliano ya Kimkakati, Itifaki, Masuala yanayohusu Ulinzi na Usalama, Usimamizi wa Fedha za Umma na Rasilimali Nyingine, Manunuzi katika Sekta ya Umma na Udhibiti wa Madawa ya Kulevya. 


Hivyo makala Wakuu wa Mikoa, Makatibu Tawala wa Mikoa Tanzania Bara Kushiriki katika Mafunzo ya Uongozi

yaani makala yote Wakuu wa Mikoa, Makatibu Tawala wa Mikoa Tanzania Bara Kushiriki katika Mafunzo ya Uongozi Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Wakuu wa Mikoa, Makatibu Tawala wa Mikoa Tanzania Bara Kushiriki katika Mafunzo ya Uongozi mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/12/wakuu-wa-mikoa-makatibu-tawala-wa-mikoa.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "Wakuu wa Mikoa, Makatibu Tawala wa Mikoa Tanzania Bara Kushiriki katika Mafunzo ya Uongozi"

Post a Comment

Loading...