Loading...

Jumia na Xiaomi kushirikiana kukuza ueneaji simu janja Afrika

Loading...
Jumia na Xiaomi kushirikiana kukuza ueneaji simu janja Afrika - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Jumia na Xiaomi kushirikiana kukuza ueneaji simu janja Afrika, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Jumia na Xiaomi kushirikiana kukuza ueneaji simu janja Afrika
link : Jumia na Xiaomi kushirikiana kukuza ueneaji simu janja Afrika

soma pia


Jumia na Xiaomi kushirikiana kukuza ueneaji simu janja Afrika

 Kushoto ni Makamu Mkuu wa Rais wa Jumia, Bw. Romain Christodoulou pamoja na Bw. Wang Xiang (kulia), Makamu Mkuu wa Rais wa kampuni ya Xiaomi wakiweka sahihi wakati wa makubaliano ya biashara katika Kongomano Kuu la Simu Duniani lililofanyika jijini Barcelona, Hispania mnamo Februari 27, 2019. 
Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Vifaa vya Kielekroniki vya Wateja wa Jumia, Sandeep Narayanan, Makamu Mkuu wa Rais wa Jumia, Bw. Romain Christodoulou, Makamu Mkuu wa Rais wa kampuni ya Xiaomi, Bw. Wang Xiang, pamoja na Makamu wa Rais wa Xiaomi, Wang Lingming wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kuingia makubaliano katika Kongomano Kuu la Simu Duniani lililofanyika jijini Barcelona, Hispania mnamo Februari 27, 2019.


· Ushirikiano huu unaifanya Xiaomi kuingia rasmi kwenye soko la mtandaoni barani Afrika kupitia Jumia, na kuwapatia fursa ya kipekee mamilioni ya wateja kuzifikia bidhaa za Xiaomi.

kampuni inayoongoza barani Afrika kwa kuuza bidhaa mtandaoni, imesaini mkataba muhimu wa ushirikiano wa kibiashara na kampuni inayoongoza kiteknolojia ya Xiaomi katika Kongamano Kuu la Simu Duniani (the Mobile World Congress) jijini Barcelona nchini Hispania, na kuwapatia fursa ya kipekee mamilioni ya Waafrika kuzifikia kwa urahisi bidhaa za Xiaomi.

Kupitia ushirikiano huu, Jumia itafungua duka maalum la Mi mtandaoni kwake na kuipatia Xiaomi fursa ya kuwafikia mamilioni ya wateja walioko mtandaoni katika nchi takribani 14 barani kote, wakati huo huo Jumia itaitambulisha rasmi simu aina ya Redmi Go (1GB + 8GB) mahsusi kwa Afrika na bidhaa nyinginezo nyingi ndani ya mwaka huu. Ushirikiano huu utapewa nguvu na juhudi za pamoja baina ya pande mbili za shughuli za kimasoko kwa mwaka wote wa 2019, kwa kutumia uwezo wa Jumia kwa kidigitali pamoja na wa kimasoko wa Xiaomi, ikijumuisha jamii ya mashabiki wa Mi. Hii ni hatua ya kwanza muhimu yenye kutia matumaini katika ushirikiano wa karibu baina ya makampuni haya mawili kwa miaka mingi ijayo.

“Ushirikiano huu ni muhimu sana kwetu, kwa kuwa ni dhahiri utakuza matumizi ya simu janja Afrika na kusaidia kuenea kwa manunuzi ya njia ya mtandaoni. Jumia na Xiaomi zote zina vinasaba sawa vya mtandao wa intaneti hivyo basi zitakuwa na kusudio moja: kutoa simu za kisasa zenye ubora wa hali ya juu na gharama nafuu huku ikiwapatia wateja namna ya kipekee ya kufanya manunuzi. Hii itazinufaisha kampuni zote mbili na zaidi ni wateja wote barani Afrika,” amesema Afisa Mtendaji Mkuu wa Jumia Tanzania, Bw. Zadok Prescott, akielezea juu ya ushirikiano huo.

“Tunaamini kwenye kufanya kazi na makampuni ambayo yana maadili sawa nasi na tunayofuraha kushirikiana na Jumia kuwafikia mashabiki wengi zaidi wa Mi Afrika nzima,” amesema Wang Xiang, Makamu Mkuu wa Rais wa Xiaomi. “Mfumo wa kuuza bidhaa kwa njia ya mtandaoni ni sehemu ya Xiaomi na tunaamini ya kwamba kufanya kazi na Jumia kutatusaidia kuleta ubunifu kwa kila mtu barani Afrika.” 

Afrika imeshuhudia kukua kwa kuingia bidhaa za kiwango cha gharama nafuu kutoka kwa makampuni ambayo yamejikita zaidi katika bei hususani kutokea China, kitu pekee ambacho ni muhimu katika kukuza matumizi ya simu za kisasa barani. Takwimu zinaonyesha kuwa ueneaji

wa simu za kisasa Afrika ulikuwa 36% kwa mwaka 2018, huku idadi hiyo inatarajiwa kufikia 66% kufikia mwaka 2025.


Hivyo makala Jumia na Xiaomi kushirikiana kukuza ueneaji simu janja Afrika

yaani makala yote Jumia na Xiaomi kushirikiana kukuza ueneaji simu janja Afrika Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Jumia na Xiaomi kushirikiana kukuza ueneaji simu janja Afrika mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/02/jumia-na-xiaomi-kushirikiana-kukuza.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "Jumia na Xiaomi kushirikiana kukuza ueneaji simu janja Afrika"

Post a Comment

Loading...