Loading...
title : 102.5 Lake FM yazindua kampeni ya kusafisha jiji la Mwanza “Ng’arisha Nzengo’
link : 102.5 Lake FM yazindua kampeni ya kusafisha jiji la Mwanza “Ng’arisha Nzengo’
102.5 Lake FM yazindua kampeni ya kusafisha jiji la Mwanza “Ng’arisha Nzengo’
Kituo cha Redio cha 102.5 Lake FM kimezindua kampeni ya kufanya usafi kwa jijini la Mwanza ijulikanayo kwa jina la Ng’arisha Nzengo, Uchafu Nuksi yenye lengo la kuufanya mji huo kuwa msafi zaidi.
Mkurugenzi wa kituo hicho Doreen Estazia Noni amesema kuwa wameamua kuanzisha kampeni hiyo ya usafi ili kuupendezesha zaidi mji huo ambao ni minongoni mwa miji mikubwa hapa nchini.Doreen amesema kuwa moja kati ya vipaumbele vya kampuni ya Lake Fm nikuhakikisha inatoa mianya ya kuiwezesha jamii kufikia kusudi la maendeleo binafsi na jamii nzima kwa ujumla.
“Neno ni la kabila ya Wasukuma lenye maana ya nyumbani, tumeamua kutumia neon hili ili kufikisha ujumbe haraka kwa wakazi wa jiji la Mwanza, kampeni hii ni endelevu kituo chetu cha redio kitaendelea kuhamasisha mpaka kufikia lengo letu,”
“Kituo chetu cha redio kimeamua kupanua wigo wake kwa kujihusisha katika masuala mbalimabli ya kijamii na kutatua changamoto mbalimbali na kuleta mtazamo chanya na si kuhabarisha na kuburudisha tu, naomba ushirikiano mkubwa kwa wadau, serikali na watu binafsi katika kufanikisha kampeni hii,” alisema Doreen.
Mbali ya 102.5 Lake FM, kampeni hiyo pia imewashirikisha wadau wengine kama Baamedas tv, Genic Studios , viongozi wa Jumuiya ya biashara ndogondogo, minada na masoko , mwenyekiti Justin Sagala, mwenyekiti wa Afya Minadani, Gosbert Lucas, katibu wa afya, Mariam Magembe, kiongozi wa wa madereva wa daladala Dede Petro, serikali na Asasi binafsi.
Wafanyakazi wa kituo cha 102.5 Lake FM na wadau wengine wakishiriki katika kampeni ya 'Ng'arisha Nzengo'. 
Wafanyakazi wa kituo cha 102.5 Lake FM na wadau wengine wakishiriki katika kampeni ya 'Ng'arisha Nzengo'.
Katibu wa wenyeviti wa mitaa jiji la Mwanza, Hamza Shido akishiriki katika kampeni hiyo ya 'Ng'arisha Nzengo' iliyoanzishwa na kituo cha redio cha 102.
Hivyo makala 102.5 Lake FM yazindua kampeni ya kusafisha jiji la Mwanza “Ng’arisha Nzengo’
yaani makala yote 102.5 Lake FM yazindua kampeni ya kusafisha jiji la Mwanza “Ng’arisha Nzengo’ Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala 102.5 Lake FM yazindua kampeni ya kusafisha jiji la Mwanza “Ng’arisha Nzengo’ mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/05/1025-lake-fm-yazindua-kampeni-ya.html
0 Response to "102.5 Lake FM yazindua kampeni ya kusafisha jiji la Mwanza “Ng’arisha Nzengo’"
Post a Comment