Loading...
title : Mavunde akutana na balozi wa uswisi nchini mjini Dodoma
link : Mavunde akutana na balozi wa uswisi nchini mjini Dodoma
Mavunde akutana na balozi wa uswisi nchini mjini Dodoma
Naibu waziri wa Kazi,Vijana ,Ajira na Watu wenye Ulemavu Ndg Anthony Mavunde leo amefanya mazungumzo na Balozi wa/ Uswisi Mh Florence Mattli katika ofisi za Wizara ya Kazi,Vijana,Ajira na Watu wenye Ulemavu mjini Dodoma juu ya namna bora ya ushirikiano kati ya Tanzania na Uswisi katika eneo la Ukuzaji Ujuzi kwa Vijana kupitia mpango unaotekelezwa na Wizara.
Balozi Mattli ameupongeza mpango wa Wizara wa utekelezaji wa Program ya Ukuzaji Ujuzi kwa Vijana nchini kupitia mafunzo stadi ambayo yana lengo la kuwajengea Vijana wa Tanzania ujuzi stahiki na hivyo kuwawezesha kuwa na sifa za kuajiriwa,Kujiajiri na kuajiri Vijana wengine.
Balozi Mattli ameahidi kushirikiana na Serikali katika kuunga mkono juhudi za Wizara katika uendeshaji wa Mafunzo ya Ufundi kwa Vijana kwa kufadhili kiasi cha Shilingi 34,000,000 USD kwa miaka 12 kwa ajili ya utekelezaji bora wa Mpango wa Ukuzaji Ujuzi kwa Vijana nchini.
Naibu waziri wa Kazi,Vijana ,Ajira na Watu wenye Ulemavu Ndg Anthony Mavunde akizungumza na Balozi wa Uswisi nchini Mh Florence Mattli katika ofisi za Wizara ya Kazi,Vijana,Ajira na Watu wenye Ulemavu mjini Dodoma
Hivyo makala Mavunde akutana na balozi wa uswisi nchini mjini Dodoma
yaani makala yote Mavunde akutana na balozi wa uswisi nchini mjini Dodoma Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Mavunde akutana na balozi wa uswisi nchini mjini Dodoma mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/06/mavunde-akutana-na-balozi-wa-uswisi.html
0 Response to "Mavunde akutana na balozi wa uswisi nchini mjini Dodoma"
Post a Comment