Loading...

LOWASSA MGENI RASMI UZINDUZI WA ALBAMU YA MARIAM KILYENYI

Loading...
LOWASSA MGENI RASMI UZINDUZI WA ALBAMU YA MARIAM KILYENYI - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa LOWASSA MGENI RASMI UZINDUZI WA ALBAMU YA MARIAM KILYENYI, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : LOWASSA MGENI RASMI UZINDUZI WA ALBAMU YA MARIAM KILYENYI
link : LOWASSA MGENI RASMI UZINDUZI WA ALBAMU YA MARIAM KILYENYI

soma pia


LOWASSA MGENI RASMI UZINDUZI WA ALBAMU YA MARIAM KILYENYI

Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa anatarajia kuwa mgeni rasmi kwenye uzinduzi wa albamu ya mwimbaji wa muziki wa Injili Mariam Kilyenyi, utakaofanyika Disemba 2, 2018 katika Kanisa la Kiinjili la Kirutheli Tanzania (KKKT)-Sinza Mapambano, jijini Dar es Salaam.

Mbali na Lowassa, waimbaji watakaosindikiza uzinduzi wa albamu hiyo inayoitwa ‘Hakimu wa Haki’ ni Bahati Bukuku, Dk Tumaini Msowoya, Tumaini Njole, Tumaini Mbembela,  Madamu Ruth ,Iren Mwamfupe, Bony Mwaitege, Margie Muliri, Juvenalista Mabuma  Edson Mwasabwite.

Akizungumza na Mwananchi, Mariam alisema amemualika Lowassa kwa sababu ndiyo aliyeanza kuibu kipaji chake, alipompa nafasi ya kuimba siku ya sherehe yake ya kuzaliwa.“Lowassa ni baba yangu, aliibua kipaji change ndio maana nikatamani awe mgeni rasmi na amekubali, namshukuru sana Mungu kwa sababu hii,” alisema.

Alitaja nyimbo zilizo kwenye albamu yake kuwa ni Hakimu wa Haki, Pam Pam tukuza, Natafuta Mshauri, Chereko leo, Nasikia Kuitwa, Agano Langu, Ushindi Lazima na Mapambazuko.“Nasikia kuitwa ndio wimbo ambao niliimba wakati nikianza mbele ya baba Lowassa, kwa hiyo ilipofika hatua ya kuandaa albamu yangu niliuweka na huo kwa sababu ndio ulionifungulia njia,” alisema.

Akizungumzia changamoto alizokutana nazo kwenye muziki huo, Mariam alisema ni gharama kubwa ya uandaaji wa muziki pamoja na kusambaza kazi hiyo.“Naimba muziki kwa sababu nasikia kuitwa kwa ajili ya kazi hiyo, kusema kweli gharama za uandaaji wa kazi nzuri ni kubwa hata hivyo namshukuru Mungu kwa sababu nimeshakamilisha hatua ya kwanza,” alisisitiza.Mwimbaji wa muziki wa Injili Mariam Kilyenyi ambaye atazindua albamu yake skiku ya tarehe 2 mwezi wa 12 mwaka huu.




Hivyo makala LOWASSA MGENI RASMI UZINDUZI WA ALBAMU YA MARIAM KILYENYI

yaani makala yote LOWASSA MGENI RASMI UZINDUZI WA ALBAMU YA MARIAM KILYENYI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala LOWASSA MGENI RASMI UZINDUZI WA ALBAMU YA MARIAM KILYENYI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/11/lowassa-mgeni-rasmi-uzinduzi-wa-albamu.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "LOWASSA MGENI RASMI UZINDUZI WA ALBAMU YA MARIAM KILYENYI"

Post a Comment

Loading...